Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, January 25, 2011

TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA LAZINDULIWA LEO


Mwimbaji wa muziki wa kizazi kimpya, Juma Kasimu 'Juma Nature' (kulia) akipeana mkono na Meneja Mkuu wa Zantel Zanzibar ambao ni wadhamini wakuu wa Tamasha la Sauti za Busara, Nahaat Mahfoudh wakati wa mkutano wa kutangaza Tamasha hilo, Dar es salaam jana katikati ni Makamu mwenyekiti wa Tamasha hilo, Simai Said

Mwimbaji wa muziki wa kizazi kimpya, Juma Kasimu 'Juma Nature' akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa kutangaza Tamasha la Sauti za Busara, Dar es salaam jana litakalofanyika mwanzoni
Februari 9-13.Juma Nature ni kati ya wasanii watakaotumbuiza katika tamasha hilo, kushoto ni Meneja Mkuu wa Zantel Zanzibar ambao ni wadhamini wakuu wa Tamasha hilo, Nahaat Mahfoudh na Makamu mwenyekiti wa Tamasha hilo, Simai Said.

Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara,Yusuf Mahmoud akizungumza katika mkutano wa ufunguzi rasmi wa tamasha hilo kwa vyombo vya habari asubuhi hii katika hoteli ya Southen Sun,jijini Dar.katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Tamasha hilo,Simai Said na kulia ni Nahaat Mahfoudh kutoka Zantel.Meneja wa Tamasha la Sauti Za Busara,Stella Stephen akizungumza katika mkutano huo.wengine ni Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel,Brian Karokola,Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti Za Busara,Yusuf Mahmoud,Makamu Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti za Busara,Simai Said na Nahaat Mahfoudh kutoka Zantel.
Baadhi ya Wanahabari na Wasanii walioshiriki katika mkutano huo.
Ankal akiwa na wadau wa Sauti Za Busara,toka shoto ni Yusuf Mahmoud,Waziri Ally, Nahaat Mahfoudh kutoka Zantel pamoja na Simai Said.

Sauti za Busara ni moja ya matamasha yenye mvuto wa kipekee barani Afrika, mwaka huu litafanyika kwa mara ya nane visiwani Zanzibar katika Mji Mkongwe kuanzia Februari 9-13.
Tamasha hili hukutanisha watu wa tamaduni mbalimbali na kuwaweka pamoja, wakisheherekea na kufahamiana kama alivyosema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete katika hotuba yake ya ufunguzi wa tamasha la mwaka 2010.

“tukio hili ni muhimu kwa kuwa linatoa fursa kwa wageni na wenyeji wa tamaduni mbalimbali kubadilishana mawazo,kuonyeshana upekee wao, utajiri na utofauti wa muziki wetu. Kwa ujumla linachangia kuimarisha muingiliano wa tamaduni na urafiki.”

Sauti za Busara huwakutanisha wasanii wakubwa wa muziki barani Afrika pamoja na kuibua vipaji vingine nchini. Mwaka huu vikundi 40 vitatumbuiza, baadhi ni, Orchestre Poly Rythmo de Cotonou (Benin), Blick Bassy (Cameroon), Otentikk Street Brothers (Mauritius), African Stars Band aka Twanga Pepeta (Tanzania), Mlimani Park Orchestra (Tanzania), Kwani Experience (South Africa), Culture Musical Club (Zanzibar), Mohamed Ilyas & Nyota Zameremeta ft. Bi Kidude (Zanzibar), Jagwa Music (Tanzania), Bismillahi Gargar (Kenya), Maulidi ya Homu ya Mtendeni (Zanzibar), Djeli Moussa Diawara (Guinea), Christine Salem (Reunion), Yaaba Funk (UK), Muthoni The Drummer Queen (Kenya), Jahazi Modern Taarab (Tanzania), Les Frères Sissoko (Senegal), Sukiafrica Sukiyaki Allstars (Pan Africa / Far East), Groove Lélé (Reunion), Vusa Mkhaya & Band (Zimbabwe / Various), Djaaka (Mozambique), Nomakanjani Arts (Zambia), Percussion Discussion Afrika (Uganda), Tunaweza Band (Tanzania), Staff Band Namasabo (Tanzania), Lelelele Africa (Kenya), Atemi & the Ma3 Band (Kenya), Sauda (Tanzania).

Sherehe za mwaka huu zitafunguliwa na maonyesho mbalimbali ya kuvutia, muziki wenye nakshi mbalimbali ikiwemo nyimbo za kiswahili, madansa, maonyesho ya vipande vya filamu za muziki kutoka Tanzania, Uganda, DRC, Ivory Coast na Senegal.

Wakati huohuo, tamasha litadhamini Busara Xtra, yaani matukio ya nje ya tamasha yatakayoandaliwa ndani ya Zanzibar na ambayo yatawavutia na kuwanufaisha wageni waalikwa.
Hii itatoa fursa kwa wasanii wa ndani kuonyesha kazi zao, kuwahamasisha wageni kuendelea kutazama maeneo mengine ya visiwa na kuongeza kipato kwa watu wengi.
Mwimbaji wa muziki wa kizazi kimpya, Juma Kasimu 'Juma Nature' (kulia) akipeana mkono na Meneja Mkuu wa Zantel Zanzibar ambao ni wadhamini wakuu wa Tamasha hilo, Nahaat Mahfoudh wakati wa mkutano wa kutangaza Tamasha hilo, Dar es salaam jana katikati ni Makamu mwenyekiti wa Tamasha hilo, Simai Said

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...