Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, November 2, 2011

KESI DHIDI YA UNYANYASAJI WA KIJINSIA TANZANIA ZAONGEZEKA


NA GLADNESS MUSHI,ARUSHA

Imeelezwa kuwa kesi dhidi ya ukatili kwa wanawake hapa nchini zimeongezeka sana tofauti na kipindi cha nyuma hali ambayo inadhirisha wazi kuwa asilimia kubwa ya wanawake wameanza kujua haki zao za msingi.

Hayo yamebainishwa mjini hapa na Bw Meshaki Ndasokii ambaye ni mkurugenzi wa maendeleo ya jinsia katika wizara ya maendeleo ya jamii na watoto,wakati akiongea na wadau mbalimbali kutoka katiika nchi za maziwa makuu.

Bw Meshaki alisema kuwa kuwepo kwa kesi nyingi kunaonesha kuwa baadhi ya wanawake ambao wananyanyaswa katika jamii wamefanikiwa kujua haki zao za msingi

Aidha ameeleza kuwa kiwango cha kesi hizo kimepanda kwa kiwango kikubwa tofauti na miaka ya nyuma ambapo kulikuwa hamna kesi nyingi dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia.

Aliongeza kuwa pamoja na kuongezeka kwa kesi nyingi sana hasa katika maeneo mbalimbali hapa nchini lakini bado kwa upande wa maziwa makuu kun a unyanyasaji mkubwa sana hali ambayo inatakiwa kuchukuliwa tahadhari ya hali ya juu sana.

Bw Meshaki alisema kuwa unyanyasaji huo unakuwa zaidi hasa kwenye nchi ambazo zina vita kubwa sana ambapo wanawake wengi hunyanyaswa kijinsia hali ambayo ina madhara makubwa sana kwa jamii hizo hasa kwa upande wa wanawake.

Awali alisema kuwa ili kukabiliana na suala hilo hasa kwenye nchi za maziwa makuu kunaitajika kuwepo na marudio ya kuridhia mikataba mbalimbali sanjari na kuchunguza hali ya unyanyasaji huo

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...