Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, October 18, 2013

PAPII KOCHA, BABU SEYA... NAFASI YA MWISHO



Na Mwandishi Wetu

KITENDO cha Mahakama ya Rufaa kukubali kusikiliza marejeo ya hukumu ya kifungo cha maisha jela katika kesi iliyokuwa ikimkabili mwanamuziki Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ kimetafsiriwa kuwa ni kama wamepata nafasi ya mwisho ya kuweza kujinasua............BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI»


WARAKA WA PAPII KOCHA
Mahakama hiyo ilikubali ombi hilo hivi karibuni na kueleza kuwa marejeo hayo yanatarajiwa kusikilizwa Oktoba 30, mwaka huu ikiwa ni miezi kadhaa baada ya Papii Kocha kutuma waraka wa kuomba msamaha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete. 



Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ndiye aliyekubali kuufikisha kwa JK hivyo kuna madai kuwa huenda waraka huo ndiyo umezaa matunda.



WARAKA UMEZAA MATUNDA?
“Unajua ule waraka ulikuwa na maneno ya kuumiza sana. Inawezekana kabisa kuwa ulimfikia JK akaagiza suala hilo liangaliwe upya. Haina maana kuwa JK anaingilia sheria. Nadhani wanasheria wana vipengele vingi ambavyo vinaruhusu marejeo ya rufaa hiyo. Kilichopo hapa ni namna ya kuzitafsiri sheria kisha kuona kama rufaa hiyo inaweza kusikilizwa.



“Ninachojua ni kwamba Babu Seya na Papii Kocha wamepata nafasi ya mwisho ya kuweza kujinasua kwa sababu hata wakili wao (Mabere Marando) yupo vizuri katika kuwatetea wateja wake.


MUNGU ANAWEZA
“Mimi naamini Mungu anaweza yote hivyo tuwaombee rufaa yao iende vizuri,” alisema mmoja wa ndugu wa familia ya Nguza.



Awali mwaka 2004, baada ya kukutwa na hatia katika kesi iliyowahusisha na ubakaji wa watoto kumi wa Shule ya Msingi, Mashujaa iliyopo Sinza, Dar, Babu Seya, Papii Kocha na wakili wao Marando waliomba marejeo ya hukumu hiyo.



JOPO LA MAJAJI
Marejeo hayo yanatarajiwa kusikilizwa na jopo la majaji watatu wa mahakama hiyo ambao ni Nathalia Kimaro, Mbarouk Mbarouk na Salum Massati. 



Katika hukumu hiyo iliyotolewa Februari 2010, mahakama hiyo iliridhia hukumu ya kifungo cha maisha kwa Babu Seya na Papii Kocha huku ikiwaachia huru watoto wawili wa Babu Seya, Nguza Mbangu na Francis Nguza.

WATIWA HATIANI


Juni 25, 2004 Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar, iliwatia hatiani Babu Seya na wanaye hao kwa kupatikana na hatia ya kubaka na kulawiti.



Januari 27, mwaka 2005, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Thomas Mihayo alitupilia mbali rufaa yao iliyokuwa ikipinga hukumu iliyotolewa na aliyekuwa Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Addy Lyamuya ambaye aliwatia hatiani kwa makosa yote waliyokuwa wameshitakiwa nayo Juni 25, mwaka 2004.



Babu Seya na wanawe walidaiwa kutenda makosa 10 ya kubaka watoto wenye umri kati ya miaka sita na minane na makosa mengine 11 ya kulawiti watoto wa kike wenye umri huohuo kati ya Aprili na Oktoba 2003.Chanzo: Global Publishers Blog

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...