Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, October 28, 2013

MTEMVU,KIMATH WAPIGA MARUFUKU MALORI KUMWAGA MAJI TAKA MABWAWA YA KURASINI,DAR


 Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu  akimuuliza swali Mfanyakazi wa  Mamlaka ya Maji Safi na Taka Dar es Salaam (DAWASA),Omar Mlanzi, walipokwenda kupiga marufuku malori kwenda kumwaga maji taka katika mabwawa ya Kurasini, Dar es Salaam, baada ya baadhi ya wakazi wa eneo hilo kulazwa hospitali kwa kuhara na kutapika kulikosababishwa na Dawasa kutoweka dawa ya kuua bakteria kwenye mabwawa hayo.Sababu nyingine ni kwamba mabwawa hayo yamezidiwa baada ya mabwawa mengine jijini kufungwa hivyo malori yote ya taka kwenda kumwaga hapo. Wa pili ni Diwani wa Kata hiyo, Wilfred Kimath na Augustino ambaye ni mtumishi wa kampuni binafsi iliyopewa jukumu la kusimamia malori yanayokmwaga mati taka katika mabwawa hayo.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mtemvu akijadiliana jambo na Diwani, Kimath
 Baadhi ya malori yaliyokutwa yakimwaga maji taka kwenye mabwawa hayo.
 Moja ya malori lililokutwa likimwaga maji taka kabla ya kupigwa marufuku

 Mtemvu akiwasiliana na uongozi wa Dawasco na Dawass
 Moja ya mabwawa likiwa limefurika maji taka kupita kiasi
 Mfanyakaziwa lori akifunga baada ya kuamriwa kufanya hivyo
 Mmoja wa madereva  Hemed Abdalah akielezea adha wanayipata baada ya mabwawa ya maji taka kufungwa jijini
 Mtemvu kulia akiangalia baadhi ya malori ya maji taka
Mtemvu na Kimath wakiondoka baada ya kufunga matumizi ya mabwawa hayo

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...