Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, October 15, 2013

MKUU WA MKOA WA RUKWA STELLA MANYANYA AMUWAKILISHA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA KATIKA HARAMBEE YA UJENZI WA KANISA LA MORAVIAN MJINI SUMBAWANGA NA KUCHANGISHA ZAIDI YA MIL. 58



Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza katika harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa kanisa la Moravian Tanzania mjini  Sumbawanga akimuwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda aliyemteua kufanya hivyo baada ya yeye kukabiliwa na majumu mengine ya kitaifa. Awali Waziri Mkuu aliafiki mualiko wa Kanisa hilo katika kuongoza harambee hiyo ambayo imefanikiwa kupata zaidi  ya Tsh. Milioni  58 zikiwepo fedha taslim zaidi ya shilingi Milioni  47 na nyingine zikiwa ni ahadi. Zimekuwepo pia ahadi za mifuko 30 ya  Cement na mlango mmoja mkubwa wa kuingilia kanisani hapo. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Stella Manyanya akitoa neno la awali kabla ya zoezi  hilo la harambee kuanza ambapo aliwaomba waumini na wageni waliofika  katika hafla hiyo kutoa kwa moyo katika kuchangia kazi hiyo ya  Mungu. Kwa kuanzia alitoa ahadi ya Waziri Mkuu aliyoitoa ambayo ni  milioni tano (5) na yeye mwenyewe kuchangia milioni moja. Aliendeleza  harambee hiyo kwa kuwachangisha kwanza viongozi wa Serikali alioambatana nao na kuendelea na taratibu zingine kwa mujibu wa ratiba.   
Askofu Mkuu Conerad Nguvumali wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Rukwa  akitoa neno katika hafla hiyo ambayo aliwataka waumini wa kanisa hilo  kuchapa kazi kwa nguvu na kuepukana na uvivu ambao alisema ni ugonjwa  mkubwa kuliko hata gonjwa la ukimwi. Alikemea pia tabia ya watu wengi  kuwahusisha watu waliofanikiwa kwa jitihada zao wenyewe na imani za  “Freemason” au “Ufisadi”. 
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Methew Sedoyyeka akizungumza katika harambee  hiyo baada ya kupewa fursa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kutoa mchango wake,  aliahidi mchango wa laki tano na mlango mmoja mkubwa wa kuingilia  kanisani hapo. 
Baadhi ya viongozi wa Serikali waliohudhuria katika hafla hiyo, kulia ni  Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga William Shimwela ambaye pia ni  mwanakamati wa ujenzi katika kanisa hilo, Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini Aeshi Hillal na nyuma yake ni Kamanda wa Polisi Mkoa  wa Rukwa Mwaruanda. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akiendelea na zoezi la uchangishaji.
Baadhi ya waumini wa kanisa la Moravian Sumbawanga wakimfagilia kwa shangwe  Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini Aeshi Hillal aliyachangia Tsh.  Milioni kumi zikiwepo za kwake binafsi Mil. 7 na nyingine Mil. 3  kuchangiwa na wabunge wenzake. Picha Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...