Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, October 13, 2013

MAKAMU WA RAIS ANOGESHA HAFLA YA CHAKULA CHA HISANI, KAMPENI YA SIMAMA KWA AJILI YA AKINAMAMA WA AFRIKA, JIJINI DAR


Meza Kuu ya viongozi katika hafla hiyo.
Makamu wa Rais, Dkt. Mhammed Gharib Bilal, aliyekuwa mgeni rasmi katika Hafla ya Chakula cha Hisani iliyoandaliwa na AMREF Tanzania kwa kushirikiana na Montage Limited na Benki M, maalum kwa ajili ya kuchangisha fedha kwa Kampeni ya Simama kwa ajili ya akinamama wa Afrika, akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 25, kutoka Kwa Mwakilishi wa Benki ya NBC, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jana usiku kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo ina lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya Kusomesha Kinamama wakunga ili kusaidia kupunguza Vifo vya Mama na Mtoto, ambapo jumla ya Sh. milioni 719 zilipatikana wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Hussein Mwinyi.
Miongoni mwa wadau waliofanikisha mkutano huo walitunukiwa vyeti vya kutambua mchango wao.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya Chakula cha Hisani ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Kampeni ya Simama kwa ajili ya akinamama wa Afrika, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana usiku. Katika hafla hiyo jumla ya Sh. milioni 719, zilipatikana. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE

Mwanafunzi Mkunga kutoka kabila la Kimasai, Toinoi Kayu Moringe (20) anayeendelea kupata elimu ya Ukunga katika Chuo cha Uuguzi na Ukunga cha Muheza cha St. Augustino, akizungumza kuto ushuhuda kuhusu elimu yake na mtazamo wa kabila lake kuhusiana na suala zima la elimu hususan kwa mtoto wa kike, wakati wa hafla ya chakula cha Hisani iliyoandaliwa na AMREF kwa kushirikiana na Kampuni ya Montage na Bank M, kwa ajili ya kuchangisha fedha za kampeni ya Simama kwa ajili ya akinamama wa Afrika, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, jana usiku.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Montage Limited, Teddy Mapunda, akizungumza na kutoa shukrani kwa Wadhamini na wahisani waliojitokeza katika Kushiriki nae kuandaa Hafla hiyo ya Usiku wa Chakula cha Hisani iliofanyika Jana usiku katika Hotel Ya Serena.
Mama Salma Kikwete, akizungumza wakati akisoma hotuba yake katika hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Bank M, Nimrod Mkono, akizungumza na kutangaza mchango wa benki hiyo wakati wa hafla hiyo, ambapo alitangaza mchango wa Sh. milioni 125.
Mama Salma Kikwete, akipokea zawadi kutoka kwa Mwakilishi wa AMREF Tanzania, Ritta Ameron, wakati wa hafla hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa mkutano huo. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...