Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, September 2, 2010

TBL YATOA MSAADA WA MILIONI 31


Mkurukenzi mkuu wa kampuni ya bia Tanzania (TBL),Robin Goetzsche (kulia) akikabidhi makubaliano ya msaada kwa wa sh. milioni 31.9 kwa Mwenyekiti wa kikundi cha wajasilia mali cha MSABI


Kampuni ya Bia Tanzania kupitia mradi wake wa maji ujulikanao kama “HAKUNA MAJI,HAKUNA UHAI” umesaini mkataba wa jumla ya shilingi million 31.9 na kikundi cha wajasiriamali cha MSABI.

Kikundi cha MSABI kinaunganisha vijana wa rika mbalimbali kutoka Ifakara. Kupitia mkataba huu kikundi cha MSABI kwa ushirikiano na Kampuni ya Bia Tanzania itashirikiana katika kuchimba visima 10 ambapo shule 10 zilizoko kwenye vijiji 5 vitafaidika.

Kazi zitakazofanywa na kikundi ni pamoja na kuongeza ujuzi wa watu wa vijiji husika katika kutengeneza, kutunza visima hivi vitakavyokuwa vinaendeshwa kwa kutumia kamba ya mikono kwa kusukuma maji. Kwa kuhakikisha maji yanayovunwa kwenye visima vitakavyochimwa ni safi na salama, mtambo wakupima ubora wa maji utanunuliwa kwenye mradi huu.

Pamoja na hayo shule nyingine mbili sitafaidika kwa kujengewa vyoo ambapo watumiaji zaidi ya mia saba wataweza kuvitumia.

Fedha hizo zinazotolewa na TBL zitawawezesha wataalamu wa MSABI kufanya kazi zilizokubalika katika vijiji vitano vya mkoa wa Morogoro navyo ni Mngeta, Namawala, Idete, Ifakara na Kiberege.

Kipaumbele cha kwanza kitatolewa katika matasisi mkubwa kama shule na hospitali za vijiji hivyo. Inategemewa kuwa vijiji husika vitashiriki kikamilifu katika kuhakikisha mradi huu unafanikiwa katika maeneo yao.

Mchango mmoja wapo unategemewa kutoka kwa wanavijijini ni pamoja na kuchangia rasilimali mbali mbali kama mchanga, nguvu mali ili kukamisha ujenzi wa visima vitakavyokuwa vinawapatia maji safi na salama katika vijiji vyao husika.

Mradi wa maji ndani ya Kampuni ya Bia Tanzania ni mradi maalumu na wenye kipaumbele kikubwa katika kampuni hii. Kwa kuona umuhimu wa maji kwa kampuni na jamii mzima Kampuni ya Bia Tanzania itawekeza zaidi ya shilling billioni 3 kwa kipindi cha miaka mitatu katika kuhakiksha upatikanaji wa maji safi na salama kwa jamii.

Akiongea wakati wa kusaini mkataba huu katika ukumbi wa mikutano wa Safari, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bwana Robin Goetzsche alisema, “ni furaha kubwa kwa Kampuni ya Bia Tanzania kuanza kutekeleza mradi huu ambao nina imani jamii kubwa itafaidika kwa kupata maji safi na salama”.

Aliendelea kusema, janga la maji lililopo mbele yetu kama inavyotabiriwa kwa mwaka 2025 ni janga kubwa kama hatutakuwa makini hivyo alihasa makampuni binafsi na vikundi mbalimbali vyenye ujuzi juu ya upatikanaji wa maji safi na salama washirikiane na serikali ili kuhakikisha kwa pamoja tunapigana na janga lililopo mbele yetu.

Pia Meneja wa mradi wa maji ndani kwa Kampuni ya Bia Tanzania bwana Phocas Lasway alisema, “Kampuni ya Bia Tanzania inatoa kiasi hiki cha fedha kwanza ili kuungana na juhudi za serikali katika kupambana na janga la maji linaloweza kutokea, pia kuwapa watu utaalamu wa kutumia na kutunza maji hasa yale ya mvua.

Ni nia ya Kampuni kufufua tena ile teknologia ya kuvuna maji ya mvua kwenye mapaa ya nyumba zetu ili kuhifadhi maji yanayopotea bure .Pamoja na hayo ni kuwawezesha wajasiriamali katika vikundi vyao kupata ajira mbalimbali iwasaidie kuongeza kipato”.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...