Marquee
tangazo
Saturday, October 16, 2010
MAPACHA WATATU WAFANYA KUFULU
Rapa wa bendi ya Frican Stars anayeitwa Furgason akicheza na mmoja wa wanenguaji wa bendi ya African Stars jana usiki wakati wa onesho la uzinduzi wa albam ya Jasho la Mtu. ZAIDI TEMBELEA http://fullshangwe.blogspot.com/
Huyu alikuwa mjamzito lakini yeye akaamua kuja kwenye onesho la mapacha watatu na hatimaye akawazaa mapacha watatu palepale Traveltine Magomeni ambao ni Josse Mara wa FM Academia, Harid Chokoraa na Kalala Jujior ambao jana walizindua albam yao ya Jasho la Mtu.
Vijana Twende Kazi! Mwanamuziki wa FM Academia Josse Mara akiongoza wanenguaji pamoja na wanamuziki wenzake wanaounda kundi la Mapacha wa3 katika kuzindua albam yao ya Jasho la Mtu ulifanyika usiku wa kuamkia leo kwenye hoteli ya Traveltine Magomeni jijini Dar es salaam ukisindikizwa na bendi ya African Stars na Mzee Yusuf kutoka Jahazi Molden Taarab.
Mzee Yusuf mwimbaji wa muziki wa Taarab na Kiongozi wa bendi ya taarab ya Jahazi Molden Taarab akiimba huku akiwa amezungukwa na vimwana jukwaani wakati aliposhiriki katika uzinduzi wa albam ya Mapacha wa3 inayoitwa Jasho la Mtu.
Mwimbaji Harid Chokoraa akionyesha uwezo wake katika kucheza wakati wa onesho la uzinduzi wa albam yao inayoitwa Jasho la Mtu kundi hilo la Mapacha wa3 lilikonga nyoyo za mashabiki na kuwakuna vilivyo usiku wa kuamkia leo kwenye hoteli ya Travltine Magomeni jijini Dar es salaam kulia ni Kalala Junio na kushoto ni Josse Marra. Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka ambaye alikuwa mgeni rasmi akizindua rasmi albam ya kundi la Mapacha WA3 inayoitwa Jasho la Mtu katika uzinduzi wa nguzu uliofanyika kwenye hoteli ya Traveltine Magomeni jijini Dar es salaam, kundi la Mapacha WA3 linaundwa na Mwanamuziki Josse Marra kutoka FM Academia, Kalala Junior na Harid Chokoraa. Katika picha kulia ni Bw. Ahmed Magoma na kushoto mwisho ni Bw. Bitusi Mkurugenzi wa B2C Transport katikati ni Masoud Wanani Mkurugenzi wa CDS wakishuhudia uzinduzi huo.
http://fullshangwe.blogspot.com/
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment