Marquee
tangazo
Thursday, October 21, 2010
MUDHIHIRI MUDHIHIR KUTUNUKIWA SHAHADA YA UDHAMILI JUMAMOSI HII
CHUO Kikuu Huria Cha Tanzania(OUT),kinatarajia kufanya mahafari yake ya 22 siku ya jumamosi, ambapo miongoni mwa watu wanaotarajia kutunukiwa shahada ya udhamili ni pamoja na aliyekuwa Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Bw. Mudhihiri Mudhihir.
Katika mahafari hayo,jumla ya wahitimu 2358 wanatarajia kutunukiwa vyeti, Stashahada, Shahada, Shahada ya Uzamili na Shahada ya Uzamivu.
Akizungumza Dar es Salaam leo Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Tolly Mbwette alisema mahafari hayo yatafanyika makao makuu ya chuo hicho yaliyoko Bungo, Kibaha Mkoa wa Pwani.
"Miongoni mwa wahitimu hao ni pamoja na Mawaziri wa zamani wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano... akiwemo waziri ambaye alipata ajali mbaya na kupoteza mkono wake, pamoja na walemavu wawili wa macho" alisema.
Alisema idadi ya wahitimu wa shahada ya kwanza imeongezeka ukilinganaisha na mwaka jana, huku kukiwa na wahitimu wa kwanza kwa Shahada ya uzamili ya Sheria na Teknolojia ya Mawasiliano.
Aidha, mahafari hayo yatatanguliwa na Kikao Cha 22 Wanazuoni kinachofanyika kesho na kutoa zawadi kwa wahitimu waliofaulu vizuri.
Kwa mujibu wa Prof. Mbwete, zawadi hizo zinazofika sh. milioni 4.5,zitatolewa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi au mwakilishi wake.
Shughuli hiyo pia itafuatiwa na mada kuhusu 'Umiliki wa Ardhi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki', itakayowasilishwa na Mkuu wa Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Profesa Palamaganda Kabudi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment