Marquee
tangazo
Thursday, October 14, 2010
SHULE YA SEKONDARI YA MASOMO YA SAYANSI YAJENGWA BAGAMOYO
SERIKALI inajenga shule ya vipaji Miono Tarafa ya Miono Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani ambayo itatumiwa na wanafunzi watakaosoma masomo ya sayansi.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bi Mwantumu Mahiza juzi alitembelea mradi wa ujenzi wa shule hiyo ambao unafadhiliwa na Ubelgiji.
Akizungumza na waandishi wa habari, Bi. Mahinza alisema kuwa shule hiyo itakwua ikichukua wanafunzi wenye vipaji maalumu vya masomo ya sayansi, inatarajiwa kukamilika mwanzoni mwakani na kufunguliwa Machi mwakani, ina uwezo wa kuchukua wanafunzi 400.
Bi. Mahinza alisema gharama za ujenzi wa shule hiyo itakayokuwa ikichukua wanafunzi mchanganyiko itakapokamilika itakuwa ni sh. bilioni 4.8.
Alisema katika kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata elimu bora, serikali tayari imetayarisha walimu wa kufundisha shule hiyo ambao wanasubiri kukamilika ili kufikana na kuanza kazi.
Mbali na ujenzi wa madarasa pia kuna mradi wa ujenzi wa nyumba za walimu, zahanati na miundombinu mingine kama supamaketi kwa ajili ya kupata mahitaji mbalimbali.
Aliwashukuru wananchi kwa kuiunga mkono serikali kwa kuitikia mwito wa ujenzi wa shule za sekondari za kata ambazo zimesaidia wanafuzi wengi wanaomaliza darasa la saba kujiunga na sekondari, kitu ambachi kimechochea uamuzi wa kujengwa shule hiyo ya vipaji maalumu.
Naye mkandarasi wa ujenzi wa shule hiyo wa Kampuni ya United Builders Ltd, Bw. Frederick Shao alisema kuwa ana imani mradi huo kukamilika kwa wakati kama ilivyopangwa kwa kuwa hakuna mvua ambayo huwa kikwazo.
Kutokana kuwepo ushirikiano mzuri na wanakijiji, alisema kampuni yao imejitolea kujenga darasa moja gharama zao kwa shule ya msingi itakayojengwa kijini hapo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment