Marquee
tangazo
Friday, October 22, 2010
TWIGA STARS KWENDA BOTSWANA
TIMU ya Taifa ya Wanawake 'Twiga Srars' inatarajiwa kuondoka nchini Jumatatu ijayo kwenda nchini Botswana kucheza mechi mbili za kirafiki.
Twiga Stars wanashiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake, ambayo inaanza kutimua vumbi wiki ijayo nchini Afrika Kusini, na Tanzania imepangwa kuanza na timu ya huko.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodger Tenga, alisema timu hiyo inatakiwa kuwasili nchini Afrika Kusini Oktoba 28 mwaka huu, lakini kabla ya kwenda huko watatakiwa kucheza mechi mbili za kirafiki.
"Tumeona ni vyema tukaitafutia timu yetu mechi mbili za kirafiki kabla ya kwenda Afrika Kusini, hivyo watacheza na timu ya taifa ya wanawake ya Botswana, kwasababu wametukubalia ombi letu," alisema Tenga.
Alisema kikosi cha wachezaji 20 na viongozi sita kitondoka Jumatatu ijayo, na Oktoba 28 viongozi wanne watakwenda Afrika Kusini kuungana na timu hiyo.
Tenga alisema jumla ya Sh.milioni 111 zinahitajika katika gharama zote za timu hiyo kuanzia Jumatatu itakapoondoka, na kwamba wanashukuru msaada wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mrisho Kikwete kuiachangia timu hiyo Sh.milioni 53 ambazo zilifanikisha kambi na posho za wachezaji.
Alisema kila Mtanzania anawajibu wa kuichangia timu ya taifa ya Wanawake, kwani ndio mara yake ya kwanza kushiriki michuano mikubwa kama hiyo.
Twiga Stars wanawania kufuvu kucheza fainali za Kombe la Mataifa, zinazotarajiwa kufanyika mwakani nchini Ujerumani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment