Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, October 12, 2010

WANAUME WADHALILISHAJI WANAWAKE KATIKA SANAA LUHIZA MBUTU APASUA


Wasanii wa kiume hususan wa muziki wa dansi ikiwa ni pamoja na wapenzi wa muziki huo wametajwa kuwa chanzo cha kuwadhalilisha wasanii wa kike hali ambayo imekuwa ikisababisha waonekane chini pia wasio na maadili ndani ya jamii.

Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa Jumatatu hii,Muimbaji mahili wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’,Luiza Mbutu alisema kwamba hali imekuwa mbaya kiasi kwamba wasanii wa kike hususan wanenguaji wamejikuta wakifanya mambo kinyume cha maadili ili kukidhi matakwa ya wasanii wa kiume na baadhi ya wapenzi wa muziki wa dansi. Akitoa mfano wa udhalilishaji huo, Luiza Mbutu alizungumzia tabia chafu ya (wapenzi wa muziki wa dansi) ‘mapedeshee’ kuwatuza fedha wanenguaji wa kike wawapo kwenye maonyesho kwa kuwawekea fedha kwenye matiti yao au makalio hali ambayo imekuwa ni ya kidhalilishaji kwa kiwango cha juu. “Wanenguaji wa kiume wamekuwa wakituzwa fedha kwa kupewa mikononi au mifukoni lakini wale wa kike wamekuwa wakiwekewa kwenye matiti na makalio kitu ambacho kimekuwa ni cha kiudhalilishaji sana” alilalamika Luiza Mbutu. Alitaja pia tabia ya wanamuziki wa kiume kwenye bendi kuponda mawazo ya wanamuziki wa kike hasa pale wanapokuwa na wazo la kutunga nyimbo hali ambayo imekuwa ikisababisha wao (wanaume) wawe wakipitisha nyimbo zao tu na kuwaacha wanawake nyuma kwenye suala la utunzi wa nyimbo. Aidha, alilalamikia baadhi ya wazazi ambao wamekuwa wakiwakataza watoto wao wa kike kushiriki kwenye shughuli za sanaa hivyo kuwafanya wawe wakitoroka usiku wa manane hivyo kushindwa kurudi majumbani baada ya kuomba hifadhi kwa wanaume hivyo kuishia kupata mimba zisizo tarajiwa na watoto wa mtaani. Kuhusu hili la kuwadhalilisha wasanii wa kike, wachangiaji wengi kwenye jukwaa walisema kwamba, rushwa za ngono zimekuwa zikisikika sana miongoni mwa wasanii wa kike na mara nyingi kimekuwa ni kikwazo kwao kupata mafanikio ya kisanaa.Walisema kwamba, kila wanapohojiwa wasanii wa kike lazima walalamikie rushwa za ngono wanazoombwa na wasanii waliokwishapata majina au wakuzaji sanaa

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...