Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, November 15, 2010

BONDIA DAVID HAYE ATETEA TAJI LAKE KWA KUMTWANGA MKTU KWA K.O


BONDIA David Haye ametetea ubingwa wake wa uzito wa juu duniani baada ya kumtwanga kwa KO raunsi ya tatu Audley Harrison katika pambano lililofranyika mjini Manchester usiku wa kukia jana.

Harrison alinyeshewa mvua ya ngumi na kusababisha refa kusimamisha pambano katika katika raunsi ya tatu.

Bonndia huyo alitumia muda mwingi wa raunsi mbili zamwanzo kujihami huku akirusha ngumi chache.

Haye mwenye miaka 30, alimudu kumwangusha Harrison mwenye miaka 39 kabla ya kutimia dakika nane.

Bingwa wa zamani wa Olimipiki Harrison awali alitamba kuwa angeweza kuibuka na ushindi lakini aliweza kurusha ngumi ya maana moja tu katika raunsi hizo tatu.

Pambano hilo lilipawa jina la 'Maadui Marafiki' ambalo lilikutanisha mabondia wa Uingereza tupu, ikiwa ni la kwanza tangu walipopigana Lennox Lewis dhidi ya Frank Bruno 1993 na Lewis kuibuka na ushindi.

Harrrison, ambaye awali alipondwa kwa kushindwa kupata mafaniki tango aliposhinda medalia ya dhahabu katika mashindano ya Olimpiki
Sydney 2000, alishindwa kuhimili ngumi kali kutoka kwa mpinzani wake na kufanya pambano kuisha katika dakika moja na sekunde 53 katika raunsi ya tatu

Mshindi haye alisema: "Nilimwambia kila mmoja nitamtwanga katika raundi tatu. Mara nilipoanza kurusha ngumi, ngumi zango zilikuwa nzuri kuliko wakati wowote.

"Nilijaraji kuwa angejitokeza na kujaribu kujituma zaidi, kwa kuwa ni no bondia mzuri wa kushmabulia kwa kushitukiza, lakini hakuweza kumaza raundi tatu.

Adam [Booth, mkufunzi wa Haye] alifurahia mafanikio ya bondia wake, akieleza kuwa alikuwa akijua kwamba angemsulubu mpinzani wake.

Harrison, maarufu kama 'A-Force', ambaye aliangushwa katika raundi ya tatu na kuhesabiswa na refa kabla kuendelea na kisha kumaliza pambano alimlaumu refa kwa kumaliza mechi hiyo mapama.


Alipoulizwa kama anakusudioa kustaafu ngumi alisema: "Ninatakiwa kukaa na kutathmini."

Aliongeza kuwa mawazo yake ya kutaka kumbaha Haye katika raunsi za mwisho yalimponza.

"Nimesikitika kwa sikupata nafasi kuonyesha mipnago yangu ya mchezo. Nilijiandaa kwa ushindi,nilikwenda nikiamini kuwa ningeweza kushinda na nilihisi kuwa ilikuwa ni wakati wangu.

Alisema pambano hilo halikuwa kama la paka na panya lakini alipigwa kwa ngumi za kushitukiza na kwamba hakuwa amekaa bila ya kufanya chochote.

Alisema mtengo wake wa kumnasa mpinzani wake haukuweza kufanya kazi kutokana ma kuwahiwa.

Harrison alikuwa na uzito mkubwa na mrefu zaidi ya mpinzani wake lakini vigezo hivyo havikumsaidia kwa kuwa mpinzani wake alikuwa na kasi ya kupiga ngumi na kutompa nafasi ya kurusha ngumi.

JUma ya mashabiki 20,000 walihudhuria mechi hiyo ilichezwa Uwanja wa MEN Arena, waliripuka kushangilia wakati Harrison aliporusha ngumi tatu kwa Haye, kabla ya upepo kumgeukia.

Refa Luis Pabon aliwaita magodia hao na kutaka kupigana raundi ya pili baada ya ya kuona wanaviziana lakini angalau Haye alipiga ngumi kali ya mkono wa kulia na kisha kupiga nyingi mbili katika raunndi hiyo kabl ya kucharuka raundi ya tatu.

Haye aliinggia ulingoniraundi ya tatu na kurusha ngumi kali ya kulia na kumuumiza Harrison. With Harrison akiwa katika kamba alibanwa na mpinzani wake ambaye alimrushia ngumi mfululizo kichwani na kuangushwa.


Harrison aliendelea kupigana na baada ya kuhesabiwa hadi nane lakini Haye kisha alimkimbilia na na kupiga ngumi kali ya kulia na kushoto kisha refa aliamua kumaliza pambano baada ya kuona harrison hajibu.

Pambano hilo lilihudhuriwa na mashabiki wengi akiwemo bingwa wa zamani wa light welter
Ricky Hatton, ambaye kabla alitabiri haye kuibuka na ushindi .


Haye, ambaye ametetea ubingwa wake wa dunia, kwa sasa inaonekana kama anaweza kufikiria kutwangana na mmoja kati ya mabondia ndugu Vitali bingwa IBF/WBO au bungwa wa WBC, Wladimir Klitschko.

Adam Booth, ambaye kocha na meneja wa Haye, alisema kuwa bondia wake hatapigana hadi Oktoka 2011.

"Wao (akina Klitschko )wanataka pambano kali na
David anataka pambano kali," alisema Booth.

"David anatarajia kustaafu Oktoba mwakani kwa hiyo hawana muda mrefu wa kuzungumza. Anaweza kupigana na Wladimir kabla ya majira ya joto na kisha Vitali baada ya majira ya joto."

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...