Marquee
tangazo
Monday, November 1, 2010
VIWANGO VYA MAAMBUKIZI YA SARATANI YA MATITI VYAONGEZEKA
Kwa kipindi cha miaka mingi, dhana ilijengeka kwamba saratani ya matiti lilikuwa ni jambo ambalo liliwaathiri zaidi wanawake kutoka bara ulaya ambao walikuwa kwenye umri wa miaka ya kati kutoka kwenye familia tajiri katika nchi zilioendelea, na kwa muda Fulani, dhana hii ilikuwa sahihi. Hata hivyo, sura ya saratani ya matiti inabadilika kwa kiwango cha waathirika kuongezeka kwa takriban mara saba katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.
“Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), kiwango cha saratani ya matiti ni asilimia 16 ya waathirika wote wa saratani duniani ambao ni wanawake, jambo ambalo linaifanya kuwa saratani iliyoenea zaidi ambayo si saratani ya ngozi, miongoni mwa wanawake wote duniani,” anaelezea Dk. Amit Thakker, Afisa Mtendaji Mkuu wa muda wa African Medical Investments plc (AMI). “Hii ni saratani inayoongoza katika kuwaathiri wanawake kwenye nchi zinazoendelea na zilizoendelea, huku saratani ya shingo ya kiazi ikifuatilia kwa karibu, na kuchukua nafasi ya pili. Takriban matukio milioni 1.3 hutokea na kutambulika kila mwaka, duniani. Barani Afrika, takriban waathirika wapya 20 kwa kila watu 100,000 yanasajiliwa na kiwango hiki kinaongezeka,” aliongeza Dk. Thakker.
Kwa mujibu wa WHO, takriban wanawake 87.9 kwa kila wanawake 100,000 nchini Uingereza walibainika kuwa na saratani ya matiti mwaka 2008, ikilinganishwa na kiwango kidogo cha wanawake 19.3 kwa kila wanawake 100,000 kwenye nchi za Afrika Mashariki. Hata hivyo, WHO inafanua kwamba idadi hii inatokana na kiwango kikubwa cha uelewa wa utambuzi wa awali nchini Uingereza, jambo ambalo si la kawaida kwenye nchi za Afrika Mashariki, ikiwemo Tanzania. Dk. Nimfa Ranido, daktari mkazi wa magonjwa ya wanawake kwenye Hospitali ya AMI, jijini Dar es Salaam anaunga mkono hoja hiyo na kusema “Saratani ya matiti inatibika lakini mara nyingi zaidi tunapata wanawake wanaofika kutibiwa huku athari za ugonjwa zikiwa zimefikia hatua za mbele zaidi. Barani Afrika, uelewa wa saratani ya matiti na utambuzi wa awali ni muhimu sana katika kupambana nayo; iwapo saratani ya matiti itabainika mapema, itakuwa rahisi zaidi kuitibu katika hatua hiyo. Wanawake wengi wa Kiafrika hawana ufahamu wa kujifanyia utambuzi wao wenyewe au jinsi ya kuwezesha matiti yao kukaguliwa, hivyo, elimu na kuongeza uelewa ni muhimu sana.”
Kwa kuwa mwezi Oktoba ni mwezi wa kuhamasisha uelewa juu ya saratani ya matiti, AMI wameamua kuendesha kampeni ya uelewa huo kupitia Hospitali na Zahanati ya Mwanamke Mwenye Afya Njema (Well Woman Clinic) jijini Dar es Salaam, Tanzania. “Sio tu kwamba mtazamo wetu ni kutoa huduma bora za afya kwa wagonjwa wetu, lakini tunataka kuwawezesha na kuwaelimisha juu ya afya zao ili waweze kubakia na afya njema kila wakati,” aliongeza Dk. Ranido.
Dk. Ranido anaeleza kwamba wanawake walio katika umri wa kati ya miaka 20 na 30 wanapaswa kuwa na ukaguzi wa matiti wa kitaalam (clinical breast exam – CBE) kama sehemu ya kawaida ya ukaguzi wao wa afya wa mara kwa mara, ambao unafanywa na mtaalam wa afya, angalau kila baada ya miaka tatu. Wanawake ambao wana zaidi ya umri wa miaka 40 wanapaswa kushauriana na daktari wao juu ratiba ya kufanya kipimo cha afya cha matiti (mammogram). “Licha ya hayo yote, ukaguzi wa matiti unaofanywa na mwanamke mwenyewe ni (breast self-exam-BSE) ni muhimu sana kwa wanawake walio katika miaka 20. Kama utakuwa na utaratibu wa kujikagua mara kwa mara, utatambua jinsi matiti yako yanavyokuwa na jinsi unavyoyahisi yakiwa katika hali ya kawaida, na utaweza kutambua dalili zozote zilizo tofauti mapema ili uweze kuzungumza na daktari wako mapema iwezekanavyo,” alisema Dk. Ranido.
Kuna dalili mbali mbali ambazo wanawake wanapaswa kuzitambua, kama vile uvimbe ndani ya matiti, mabadiliko ya umbo na ukubwa wa titi, na ni muhimu sana kuongea na daktari wako iwapo utakuwa na shaka au maswali yoyote kuhusu afya ya matiti yako.
“Katika jitihada zetu za kuongeza uelewa wa saratani ya matiti miongoni mwa wanawake barani Afrika, Zahanati yetu ya Mwanamke Mwenye Afya Njema itatoa huduma zilizopunguzwa gharama kwa kipimo cha mammogram kwenye miezi ya Oktoba na Novemba mwaka huu. African Medical Investments ni wabia na washirika wako katika vita dhidi ya saratani ya matiti,” anahitimisha Dk Thakker.
Kwa taarifa zaidi kuhusu African Medical Investments, tafadhali tembelea tovuti yao kwenye anuani website at www.amiplc.com
Wasiliana na: African Medical Investments
Dr Rajiv Rao
Clinical Manager
+255 22260 2500
rajiv.rao@amiplc.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment