Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, November 22, 2010

TIMU YA TAIFA YA POOL YACHEMSHA MASHINDANO YA DUNIA YAJIPA MATUMAINI KUFANYA VIZURI MWAKANI


MASHINDANO YA DUNIA UFARANSA 2010 (WORLD BLACK BALL CHAMPIONSHIP- FRANCE-2010).

Dar es Salaam, : Chama cha mchezo wa Pool Table Tanzania (TANZANIA POOL ASSOCIATION- TAPA) kwa kushirikiana na mdhamini mkuu wa mchezo wa pool table Tanzania Bia ya Safari Lager, inayozalishwa na Tanzania Breweries Limited (TBL) tunatoa rasmi taarifa na matokeo ya timu yetu taifa kwenye mashindano ya Dunia yaliyofanyika katika Ukumbi wa hotel ya Cheops iliyoko katika mji wa Limoges nchini Ufaransa.

Mashindano yalianza tarehe 08.11.2010 mpaka tarehe 13.11.2010 kwa kushirikisha nchi 12 badala ya nchi 32 kama ilivyokuwa imetarjiwa mwanzo. Sababu ya nchi nyingine kutohudhulia ni baada ya kukosa wadhamini wa kuwalipia gharama za ushiriki.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu mkuu wa chama cha pool Tanzania, Amos Kafwinga alisema; Timu yetu haikuweza kufanya vizuri sana baada ya kushika nafasi ya 10 kati ya nchi 12 zilizoshiriki ( nchi zilizoshiriki ni wenyeji France, N. Ireland, S. Ireland, Catalonia (Spain), S. Africa, England, Wales, Gibraltar, Scotland, Tanzania, Libya na Morocco) lakini tumeweza kupanda kiwango cha ubora wa nchi kutoka namba ya 16 mwaka 2008 mpaka namba ya 12 mwaka 2010 haya ni mafanikio makubwa yanayoonyesha wapi tunakwenda kupitia udhamini wa Bia ya Safari Lager.

Mwenyekiti wa chama cha pool Tanzania (TAPA), Isack Togocho; kwa niaba ya Chama Cha Pool Tanzania alitoa shukurani zake za dhati kwa Bia ya Safari Lager kuweza kufanikisha safari ya timu ya taifa na kuhakikisha mchezo wetu wa Pool unaendelea kukuwa na kupata hadhi ya juu hapa nchini. Pia aliwapongeza sana mkurungezi wa masoko wa TBL Ndugu, David Minja na meneja wa Bia ya Safari Lager Ndugu Fimbo Butallah na kampuni ya promotion ya Integrated Communication kwa kuweza kufanikisha safari ya timu ya taifa katika mashindano ya dunia mwaka huu.
Kwa kweli TBL kupitia BIA yake ya SAFARI LAGER wamekuwa Ni mfano mzuri katika udhamini Kwa kutekeleza ahadi Na kutoa ushirikiano mkubwa katika mchezo huu, na hivi leo mchezo wa Pool umekuwa na taswira tofauti na yenye matumaini makubwa hapa nchini na kuifanya nchi yetu ijulikane kimataifa kupitia mchezo huu wa pool table.

Leo hii kwa kupitia mchezo wa pool raisi wa dunia wa mchezo pool ametuomba tumwalike kwenye mashindano yetu ya Taifa ya pool mwaka 2011..

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...