Alisema warembo watakaoshiriki wanatarajiwa kuanza kujinoa Mei 29 katika ukumbi huo huku mkufunzi aliyebobea katika masuala hayo Caroline Zayumba akitarajiwa kuendesha zoezi hilo.
.”Kwa kweli tumejipanga kuhakikisha tunatoa mrembo ambaye atarudisha hadhi ya mkoa wa Lindi kama miaka iliyopita, warembo tulionao wote ni bomba, pia tunaomba wadhamini wajitokeze kwa wingi kutusaidia”, Alisema.
Mratibu huyo alisema mpaka sasa makampuni yaliyojitokeza kudhamini ni pamoja na Vodacom, Ndanda Spring Water, Muhsin General Enteroprises, Live Trading Center, Pride Fm na Lindi Oceanic hotel.
Taji la Miss Lindi linashikiliwa na Mary Adam pichani kushoto.
No comments:
Post a Comment