Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe, akizungumza katika mkutano huo kuhusu maandalizi ya Tour hiyo. Kutoka kulia ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa TBL, Edith Mushi, Mratibu wa Tuzo za Kili Muziki, Angelo Luhala na God Kusaga wa Prime Promotion. (PICHA ZOTE NA KAMANDA MWAIKENDA) KILIMANJARO PREMIUM LAGER NA BASATA WATANGAZA RASMI SAFARI ZA WASHINDI WA TUNZO ZA MUZIKI TANZANIA 2011. KILIMANJARO PREMIUM LAGER na BASATA leo wametangaza rasmi safari ya washindi wa Tunzo za Muziki 2011. Baada ya Mchakato wa Tunzo za Muziki za Tanzania zinazojulikana kama Kilimanjaro Tanzania Music Awards zilizokuwa na mafanikio makubwa Mwaka huu, Kampuni ya Bia Tanzania kupitia bia yake ya Kilimanjaro premium Lager imeona ni vyema kuwapa fursa Wasanii walioibuka washindi pamoja na baadhi ya wateule kufanya matamasha ya muziki katika baadhi ya mikoa ya Tanzania kama ishara ya shukrani kwa wapiga kura wao. Ratiba ya Kilimanjaro Tanzania Music Awards Winners Tour 2011 ni kama ifuatavyo. Tarehe Mkoa Mahali Kiingilio 07/05/2011 Dar es salaam Viwanja vya posta K’Nyama 5,000/= 14/ 05/2011 Dodoma Royal Village 5,000/= 21/05/2011 Mwanza CCM Kirumba 3,000/= 28/05/2011 Moshi Viwanja vya Chuo Cha Ushirika 2,000/= 04/06/2011 Mbeya Uwanja wa Sokoine 2,000/=
Wasanii wa Muziki walioibuka Washindi wa Tunzo za 2011 1. 20% 2. Mapacha Watatu 3. Mpoki 4. Joh Makini 5. Hard Man 6. C Pwaa 7. Khalid Chokoraa 8. Lady Jay Dee 9. Linah 10. Barnaba 11. JCB 12. Jahazi Modern Taarab 13. Ben Po Baadhi ya Wateule 1. Godzilla 2. Sam wa Ukweli 3. Mwasiti 4. Mataluma. Wawezeshaji: Kilimanjaro Premium Lager inaendelea kufanya kazi na makampuni mbalimbali katika katika kufanikisha safari hizi . Makampuni haya ni pamoja na: 1. Prime Time Promotion – Wasimamizi wakuu wa safari za Mbeya, Dodoma, Mwanza na Moshi. 2. Entertainment Masters – Wasimamizi wa Shughuli ya Dar . Maelezo ya ziada: Mwaka huu Kilimanjaro kama mdhamini imeamua kuwarudishia wadau na wapenzi wa muziki wa Tanzania Safari za Shukrani. Kwa Tamasha la Jumamosi Viwanja vya Posta Kijitomasha hapa Dar es salaam litasindikizwa na Wateule wa wimbo bora wa Afrika Mashariki Radio and Weisal pamoja na Bebe Cool kutoka Uganda.
No comments:
Post a Comment