Juni Mosi, mwaka huu kwenye ukumbi wa Hoteli ya Kitalii ya Gold Crest iliyopo
katika jengo la PPF, katikati ya Jiji la Mwanza.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Sisi Entertainment, waandaaji wa shindano
hilo, John Dotto, uzinduzi huo utaambatana na utambulisho wa warembo
watakaochuana katika kinyang’anyiro hicho.
Alisema kuwa tayari warembo wameshaanza kujiandikisha kuwania Umalkia wa Mwanza
na kwamba wanaojiona kuwa na sifa za kushiriki mashindano hayo, wanakaribishwa
ambapo fomu zinapatikana katika ofisi za hoteli hiyo.
“Bado tunakaribisha warembo wenye sifa kujiandikisha kwa sasa kwani baada ya
uzinduzi, hatutapokea mrembo yeyote yule, hata awe na sifa kiasi gani,” alisema.
Alisema kuwa shindano lao linatarajiwa kuwa la kiwango cha juu, kuanzia
maandalizi yake, warembo na shoo ya kilele cha kinyang’anyiro hicho.
Dotto alisema kwamba lengo lao mwaka huu ni kumtoa Miss Tanzania kama ilivyokuwa
miaka ya 2008 na 2009, wakiamini hilo linawezekana kutokana na jinsi
walivyojipanga.
Warembo waliotokea Mwanza na kutwaa taji la Miss Tanzania na miaka yao katika
mabano, ni Nasreen Karim (2008) na Miriam Gerald (2009) ambao walikatisha
kutamba kwa Jiji la Dar es Salaam katika mashindano hayo kutokana na kutwaa taji
la Miss Tanzania mara nyingi zaidi.
Dotto alisema: “Wadhamini wanaendelea kujitokeza na kwamba hadi sasa tunao PSI,
Vodacom Tanzania na Redd’s, wengine wanakaribishwa kujitokeza kudhamini shindano
hilo lenye historia ya kutoa Mrembo wa Taifa kwa miaka mwili mfululizo, 2008 na
2009.”http://mamapipiro.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment