
Mtabili maarufu wa nyota nchini, Shekh Yahya Husein amefariki Dunia leo saa tano kasoro robo (4:45) asubuhi njiani akiwahishwa katika Hospitali ya Mount Ukombozi Moroko jijini Dar es Salaam
Akizungumza na Mtandao huu Daktari wa zamu wa Hospitali hiyo,DK.Lehani Salum alisema alifukishwa katika Hospitali hiyo akiwa ameshafariki lakini kwa presha za Watoto wake wasingeweza kutambua.
Mtoto wa marehemu,Hassan Yahya alisema shughuli za mazishi zitakuwa kesho kwenye makabu ya Tambaza mchana saa saba na kabla ya hapo watakuwa nyumbani kwake Magomeni
Marehemu Shekh Yahya ameacha Mjane na Watoto zaidi ya 20 na wajukuu ambao hawajulikani idadi yao.

Ndugu jamaa na marafiki wa familia wakimfariji Mke wa marehemu wa pili kushoto.


Wakielekea msibani


Ndugu jamaa na marafiki wakiwa msibani

Shekh wa Mkoa na Mtoto wa marehemu


Shekh wa Mkoa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu taratibu za mazishi

Mwili wa marehemu ukihamishwa kutoka kwenye Hospitali ya Mount Ukombozi kuelekea Msikitini kwa kuhifadhi zaidi


Wakihamisha mwili wa Shekh Yahya
No comments:
Post a Comment