Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Serengeti (SBL), Richard Wells akikabidhi mfano wa hundi kwa Katibu Mkuu wa CECAFA Nicolous Musonye aliyesimama katikati ni Mwenyekiti wa CECAFA ambaye pia ni Rais wa TFF, Leodgar Tenga
TIMU 11 zimethibitisha kushirikia katika mashindano ya Kombe la CECAFA Tusker Challenge 2011 itakayoanza kutimua vumbi Novemba 25 hadi Desemba 10 mwaka huu itakayochezwa katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Nchi ambazo zimethibitisha kushiriki ni pamoja na Ethiopia, Kenya, Uganda, Rwanda, , Burundi , Djibouti, Somalia, Sudan, Zanzibar, Eritrea na Tanzanzania.Aidha jina la timu alikwa katika michuano hiyo litatangazwa baadaye.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo asubuhi katika hoteli ya New Africa Jijini Dar es Salaam , Mwenyekiti wa CECAFA ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Leodgar Tenga alisema mafanikia ya michuano ya CECAFA yanachangia ukuaji wa soka nchini , hivyo amewataka wananchi , wachezaji na wapenda michezo nchini wote kwa ujumla kutoa sapoti ya kutosha katika michuano hiyo.
“Nachukua fursa hii kuwashukuru wadhamini wetu ambao ni SBL tuliosaini mkataba wa miaka mitatu ,waliotudhamini kwa kupitia kupitia kinywaji chake cha Tusker , uzuri wa mashindano ya mwaka huu yamekutana na maadhimisho ya miaka 50 Uhuru ambapo sina budi ni jukumu la wachezaji wetu kuudhihirishia umma kwamba soka letu linaendelea kukua kwa kushiriki vyema katika michuano hii” alisema Tenga.
Aidha Tenga aliongeza kwa kusema kuwa licha ya kuwa Tanzania imeshiriki katika michuano mingi lakini ukweli ni kwamba bado tuko nyuma hivyo ametaka jitihada zaidi ziongezwe ili soka la bongo liweze kusonga mbele hasa katika ngazi ya Kimataifa Sudan ndiyo nchi pekee iliyoweza kwenda mbele katika michuano ya kuwania Kombe la Dunia.
Tenga ametoa wito kwa Kampuni mbalimbali kujitokeza katika kuongeza udhamini kwani walitamani michuano hiyo ichezwe katika miji mbalimbali hapa nchini ili Watanzania waweze kujionea kandanda safi sambamba na kusherehekea miaka 50 ya Uhuru.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi mfano wa hundi ,Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Serengeti (SBL) Richard Wells alitangaza mbele ya wandishi wa habari kwamba udhamini uliotolewa na Kampuni yake ni wa miaka mitatu ambapo mwaka huu itakuwa ni mara ya pili huku akisema kiasi walichodhamini mashindano ya Kombe la CECAFA Tusker Challenge mwaka huu ni sh. Mil.823.
Wells alifafanua kwamba udhamini huo utajumuisha gharama na mahitaji kama vile tiketi za ndege kwa msafara wote wa viongozi na wachezaji katika michuano ya CECAFA, malazi, usafiri wa magari hapa nchini, kuratibu mikutano na waandishi wa habari na mahitaji mengine ya utawala.
Aidha Wells alisisitiza kabla ya kukabidhi humba hii ni moja wapo ya malengo yaliyowekwa na Kampuni hiyo yakiwa na nia ya kukuza na kunedeleza mchezo huu nchini , vile vile kukuza na kuinua vipaji vilivyopo katika ukanda wa Afrika Mashariki na Magharibi, kwa kupitia udhamini huu unadhihirisha masimamo wa SBL kuwa Kampuni inayowajibika kwa jamii inayozunguka nchini na nchi jirani za kiafrika.
“Tunajivunia kuwa wadhamini wakuu wa CECAFA na tunashukuru kupewa heshima hii na CECAFA pamoja na Shirikisho la Soka nchini (TFF).Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Kampuni ya bia ya Serengeti kudhamini mashindano haya, mwaka jana SBL ilitumia kiasi cha sh. mil.675, ambapo timu ya Taifa, Tanzania Bara Kilimanjaro Stars iliibuka mshindi.
Wakati huohuo Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano Teddy Mapunda alitoa shukrani zake kwa Serikali kutokana na ushirikiano wake waliouonyesha na Kampuni SBL na TFF kwa ujumla katika mashindano ya mwaka jana na anaimani kubwa kwamba michuano ya mwaka huu itafana hivyo ametaka ushirikiano huo uendelee ipasavyo.
“Watanzania walitushirikiana nasi mwaka jana mwanzo hadi mwisho hivyo tunaomba na mwaka huu umoja ule uzidi nguvu, pia ni wajibu wetu tukumbuke kuwa Kombe liko nyumbani hivyo tutetee ushindi wetu ili Kombe libaki nyumbani” alisema Mapunda.
Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano Teddy Mapunda akizungumza katika hafla hiyo.Wanahabari wakiwa katika mkutano huo leo asubuhi.
Mwenyekiti wa Kampuni ya Bia Serengeti Mark Bomamni akijadili jambo na Mkurugenzi wa SBL,Richard Wells.
Mwenyekiti wa SBL , Mark Bomani akizungumza kuhuzu udhamini huo ambapo amesema Kampuni hiyo inayodhamini michezo , muziki, masuala ya kijamii sasa inampango wa kujikita katika masuala ya kilimo. Kulia ni Mkurugenzi wa SBL Richard Wells akimsikiliza Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano Teddy alipokuwa akizungumza katika mkutano huo.
Kushoto ni Mwenyekiti wa CECAFA na Rais wa TFF , Leodgar Tenga na Katibu Mkuu wa CECAFA Nicolous Musonye.
Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa CECAFA Nicolous Musonye, Mwenyekiti CECAFA Leodgar Tenga, Mwenyekiti SBL Mark Bomani, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL ,Richard Wells, Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano Teddy Mapunda na Meneja wa Bia ya Tusker Rita Mchaki.
PICHA KWA HISANI YA MTANDAO WA http://bongoweekend.blogspot.com
No comments:
Post a Comment