Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, November 2, 2011

Tenga azijia juu Klabu zilizotishia kugomea Ligi Kuu


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodgar Tenga ameibuka na kuzitaka klabu zilizotishia kugoma, ziondoe tishio hilo kwani hayo siyo makubaliano yao.

Rais huyo wa TFF, amesisitiza kuwa, Kamati ya Ligi iliyoundwa ambayo ina wajumbe 10 imeshaanza kazi na kwamba Watanzania wasiwe na wasiwasi juu ya hilo kila kitu kitakwenda kama kilivyoadhimiwa katika Azimio la Bagamoyo na kupitishwa na Mkutano Mkuu wa shirikisho hilo.

Tenga amesema Kamati ya Utendaji imetekeleza agizo la mkutano mkuu ambao ulitaka iundwe kamati maalum ya kusimamia ligi hiyo.

Amesema katika kuhakikisha kamati hiyo inafanya kazi vizuri kama inavyopaswa, ametuma maombi Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), kuwaandalia semina itakayowasaidia kupata mpangilio wa masoko ili waongoze ligi vizuri.

Amezitolea mfano nchi za Ujerumani, Sudan, Tunisia, Ivory Coast na Morocco, kuwa, haziendeeshi ligi kwa kutumia mfumo wa kampuni, lakini zina maendeleo makubwa katika soka.

Katika kikao cha klabu zinazoshiriki ligi hiyo kilichofanyika Oktoba 21, mwaka huu jijini Dar es Salaam, ziliazimia kuigomea ligi hiyo mpaka malimbikizo ya madeni yao yalipwe, pia waliitaka TFF isifanye tena mazungumzo na mdhamini wa ligi hiyo na tayari mchakato wa usajili wa kampuni umeanza, hivyo wataendesha wenyewe.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...