Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, November 2, 2011

Simba, Moro United kupigwa Chamazi LEO



MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Moro United sasa itafanyika kesho, Novemba 02, 2011 saa 10 katika Uwanja wa Azam, Chamazi jijini Dar es Salaam.

Awali mechi hiyo ilikuwa imepangwa kufanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam lakini imehamishwa kwa vile uwanja huo utatumika kwa shughuli nyingine siku hiyo.

Simba Sports Club inawaomba wanachama na wapenzi wake kujitokeza kwa wingi kuhudhuria pambano hilo kesho.

Imetolewa na

Ezekiel Kamwaga
Msemaji
Simba Sports Club

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...