Afisa Uhusiano wa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel ,Jane Matinde akikabidhi vitabu kwa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Siha,Bw.Rashid Kitambulo,kwa niaba ya shule nne zilizokabidhiwa vitabu hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni moja kwa kila shule,shule hizo ni Oshara,Magadini,Kilingi pamoja na shule ya sekondari ya Namwai,zilizoko Wilaya ya Siha,Mkoani Kilimanjaro,(kulia) ni Mkuu wa shule ya Sekonri ya Oshara, Bw.Elieta Kaaya pamoja na meneja mauzo wa Airtel bw. Pascal Bikomagu.hafla hiyo ya makabidhiano iliyofanyika shule ya sekondari Oshara jana.
Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Oshara Elieta Kaaya na wanafunzi Reina Kileo na Joseph Mwita kwa pamoja wakipokea vitabu toka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Siha,Bw.Rashid Kitambulo vilivyotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel chini ya mpango wake wa shule yetu Akishuhudia makabithiano hayo ni Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde.katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika shule ya sekondari Oshara jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Siha,Bw.Rashid Kitambulo akizungumza na kuishukuru kampuni ya Airtel kwa msaada mkubwa wa vitabu ilioutoa kwa shule nne za sekondari zailizopo wilayani hapo, mwisho kushoto ni Mwalimu mkuu wa sekondari ya Oshara Elieta Kaaya akifatiwa na wawakilishi wa Airtel Pascal Bikomagu na Jane matinde (kulia) ni Afisa Elimu Taaluma wa sekondari Wilaya ya Siha,Bw. Mussa Shaban Ally.hafla hiyo ya makabidhiano iliyofanyika shule ya sekondari Oshara jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Siha,Bw.Rashid
Kitambulo(kulia) akimkabithi vitabu kwa Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Namwai Humphrey Kirumbuyo(mwenye suti) na wanafunzi Felister Mwanga na Hamidu Yusuph Lule msaada uliotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel chini ya mpango wake wa shule yetu, Akishuhudia makabithiano hayo ni Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde. hafla hiyo ya makabidhiano iliyofanyika shule ya sekondari Oshara jana.
No comments:
Post a Comment