Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, January 12, 2012

TWIGA STARS YATAKIWA KUSHINDA WINDHOEK


Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu ameitaka timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars) kuhakikisha inabuka na ushindi kwenye mechi yake dhidi ya Namibia.
Mechi hiyo ya kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) itachezwa Januari 14 mwaka huu jijini Windhoek, Nambia na timu hizo zitarudiana Januari 29 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Waziri ametoa mwito huo leo mchana (Januari 11 mwaka huu) katika hafla fupi ya kuiaga timu hiyo na kuikabidhi Bendera ya Taifa iliyofanyika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Timu hiyo yenye msafara wa watu 25 inaondoka leo saa 2 usiku (Januari 11 mwaka huu) kwa ndege ya PrecisionAir kupitia Johannesburg, Afrika Kusini ambapo kesho alfajiri (Januari 12 mwaka huu) itaunganisha safari hiyo kwa ndege ya Air Namibia hadi Windhoek.
Wachezaji walioko kwenye kikosi hicho ni Asha Rashid, Aziza Mwadini, Ettoe Mlenzi, Fadhila Hamad, Fatuma Bushiri, Fatuma Khatib, Fatuma Mustapha, Fatuma Omari, Maimuna Said, Mwajuma Abdallah, Mwanahamisi Omari, Mwanaidi Hamisi, Mwapewa Mtumwa, Pulkaria Charaji, Rukia Hamisi, Siajabu Hassan, Semeni Abeid, Sophia Mwasikili na Zena Khamisi.
Benchi la Ufundi lina Kocha Mkuu Charles Boniface, Kocha Msaidizi Nasra Mohamed, daktari wa timu Dk. Christina Luambano na Meneja wa timu Furaha Francis.
Kiongozi wa msafara ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Lina Mhando na Naibu kiongozi wa msafara ni mjumbe wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Layla Abdallah.
Timu hiyo itarejea alfajiri ya Januari 16 mwaka huu kwa ndege ya PrecisionAir.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...