Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, January 29, 2012

WAZIRI MKUU KUKUTANA NA MADAKTARI JUMAPILI


WAZIRI MKUU Mizengo Pinda leo (Jumapili, Januari 29, 2012) atakutana na madaktari waliofanya mgomo kwenye ukumbi wa Karimjee kuanzia saa 4:00 asubuhi.
Madaktari hao kwa nyakati tofauti wamekuwa wanaomba kuonana na Waziri Mkuu na mara zote Waziri Mkuu amekubali kuonana nao lakini hawakutokea. Pamoja na kukubali huko kwa Waziri Mkuu, tarehe 25 Januari 2012 katika Mkutano wake na Wahariri wa Vyombo vya Habari aliwaomba Madaktari kuwa alikuwa tayari kuonana nao lakini hawakutokea.
Ili kuendeleza jitihada za kutaka kuonana na madaktari hao, Waziri Mkuu alituma Uongozi wa Serikali ukiongozwa na Mawaziri wa Afya na Ustawi wa Jamii; na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kuonana na Madaktari kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Starlight tarehe 27 Januari 2012. Kwenye Mkutano huo madaktari waliwasilisha malalamiko yao na kuomba kuonana na Waziri Mkuu. Kufuatia maombi hayo, Waziri Mkuu amewaandikia madaktari hao barua ya kuwataka kuonana nao leo, tarehe 29 Januari 2012 kwenye Ukumbi wa Karimjee, saa 4:00 asubuhi.
Kabla ya kufikia uamuzi huo, kulikuwa na mawasiliano kati ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Uongozi wa Medical Association of Tanzania (MAT) na baadaye Mwenyekiti wa Muda wa Kamati ya Madaktari kuhusu mgomo wa Madaktari unaoendelea.
Aidha, Viongozi mbalimbali wa Serikali wamefanya mazungumzo na Wawakilishi wa Madaktari na Madaktari wenyewe kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Starlight ili kuweza kupata ufumbuzi wa matatizo yaliyowasilishwa Ofisi ya Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu anawasihi Madaktari wote kuhudhuria mkutano.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...