Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, October 8, 2013

CHEKA KWENDA MUHEZA TANGA IDD ALHAJI KUHAMASISHA MCHEZO WA NGUMI


KOCHA WA MCHEZO wa ngumi Wilaya ya muheza Mkoa wa Tanga Carles Muhiru amempatia bondia Fransic Cheka Muhariko wa kwenda kuhamasisha mchezo wa ngumi siku ya idd alhaji katika viwanja vya jitegemee muheza ambapo siku hiyo kutakuwa na mapambano ya ngumi

ambapo yeye atakuja kuwamasisha vijana ili waweze kusonga mbele na mchezo huo ili waweze kufanya vizuri na kuliletea sifa taifa kama alivyofanya yeye

akizungumza na blog ya Super D kutoka muheza Mkoa wa Tanga Muhiru amesema unajua mimi namfundisha Cheka mazoezi ya ziada sasa hapa kwangu wanamsikia mimi namfundisha bingwa huyu sasa nimeamua kumpa mwaliko ili aje hapa watu wamuone kuwa ni yule cheka aliyechukuwa ubingwa wa WBF kwa kumtwanga Mmarekani

Muhiru alitoa rai kwa wadau kujitokeza kusapoti mchezo wa ngumi kwa njia moja au nyingine kwa kuwa mchezo huo unapendwa na vijana wengi wanaofanya  vizuri inaweza kuwa ni ajira nzuri kwa vijana kama ilivyo kwa bonia Fransic Cheka ambaye amekuwa akiwakilisha mkoa wa Morogoro ambapo kwa sasa yeye ni bingwa wa Dunia 

Pia ali karibisha Bungeni Dodoma kushudia shughuli za bunge na alipotoka bungeni alipewa zawadi nzuri na mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendera kwa kumpatia Kiwanja pamoja na Tani mbili za saruji pamoja na mabati kwa ajili ya kutengeneza nyuma ata hivyo kwa kuchekuwa ubingwa huo cheka kumemuwezesha kupatiwa viwanja viwili kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya kisasa na serekali ya mkoa huo

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...