Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, October 1, 2013

Baada ya kutamba na Uyoga msanii wa filamu Rich Richie sasa ana mbili kwa mpigo
MUIGIZAJI nyota ambaye pia ni mtayarishaji na muongozaji wa filamu, Single Mtambalike 'Richie' baada ya kutamba sana na filamu ya Uyoga aliyemshirikisha msanii Yvonne Cherryl 'Monalisa' sasa  yupo njia panda asijue ni filamu ipi kati ya mbili mpya alizozikamilisha kwa mkupuo aanze kuiingiza sokoni.
Filamu hiyo alizofyatua mkali huyo aliyeewahi kutamba na michezo ya runinga kupitia vituo vya televisheni vya CTN na ITV, ni 'Kitendawili' na 'Likizo Hii'.
Richie alisema hajui hadi sasa filamu ipi kati ya hizo aanze kuingiza sokoni kutokana na zote kuwa bomba kwa ujumbe wake na namna washiriki wake walivyozitendea haki.
"Kwa kweli nipo njia panda mpaka sasa sijui nianze na 'Kitendawili' au 'Likizo Hii' ambazo nimezikamilisha hivi karibuni na zote zimechezwa na wasanii nyota nchini," alisema Richie.
Aliwataja baadhi ya wasanii waliozishiriki filamu hizo ni pamoja na Mzee Majuto, Chuchu Hans, Maringo Saba, Baba Haji na wengine.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...