Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, September 2, 2010

WAIISLAM WATOA TAMKO BAADA YA MMOJA KUFUNGWA MIEZI SITA KWA KUVAA BARAGRASHIA





Mwenyekiti Kamati ya Vijana wa Kiislam BAKWATA Taifa, Alhaj Dr.Seif Sulle (kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuusu tamko la hukumu ya hakimu Wilbaforce Luhwaga dhidi ya Bw. Ally Sururu katika mahakama ya Wilaya ya Ilala ya kumuhukumu kwenda jela miezi sita kwa kosa la kuvaa baraghashia kushoto ni Katimu wa kamati hiyo Bw. Omary Msinzia
BARAZA KUU LA WAISLAMU WA TANZANIA
(BAKWATA)

TAMKO LA KUHUSU HUKUMU YA HAKIMU WILBAFORCE LUHWAGA DHIDI YA
BWANA ALLY SURURU KATIKA MAHAKAMA YA WILAYA ILALA

Kamati ya Umoja wa Vijana wa Kiislamu Tanzania, kwa niaba ya Mh.e Mufti Sheikh Mkuu wa Tanzania na waislamu wote kwa ujumla, tumepokea kwa masikitiko makubwa kabisa taarifa ya hukumu iliyotolewa na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya Ilala aliyetajwa kwa jina la Wilbaforce Luhwago.

Kamati ya Vijana wa Kiislamu nchini na Waislamu kwa ujumla baada ya kuisoma taarifa hiyo iliyoripotiwa kupitia chombo cha habari cha Gazeti la Mwananchi toleo Na. 03724 la tarehe 1 Septemba 2010, ilifanya juhudi za makusudi kupitia kwa Wanasheria wetu ili kufahamu ukweli wa jambo hilo. Hata hivyo kamati yetu imegundua kuwepo kwa tukio hilo ambalo kamati kupitia kwa Wanasheria watu, imebaini kuwa Hakimu huyo alivunja sheria kwa kumtaka mshitakiwa Bw. Ally Sururu avue kofia akiwa kizimbani. Amri hii dhidi ya Mshitakiwa ilikuwa ni utovu wa adabu uliyofanywa na Hakimu huyo dhidi ya Waislamu na Uislamu.

Hata hivyo Hakimu Luhwago alivunja sheria na kumnyanyasa na kumnyima uhuru wake wa kuabudu Bw. Ally Sururu. Kwa kuwa Hakimu Luhwago ametoa hukumu ya kifungo cha miezi sita kwa kosa la kujibizana na mshtakiwa alipokataa kutekeleza amri yake, vijana na waislamu nchini wameipokea hukumu hiyo kama hukumu dhidi ya mavazi ya Kiislamu mbele ya Hakimu huyo.

Aidha kamati ya vijana, Baraza na Waislamu kwa ujumla tunatoa tamko hili, kulaani vikali hukumu hiyo na tunaitaka mamlaka husika kufuatilia kwa karibu na haraka hukumu hiyo kisha kuitolea tamko kama ilikuwa hukumu sahihi.

Kamati ya vijana na Waislamu nchini tunaamini kuwa hukumu hiyo ni ya dhuluma na iliyojaa uonevu kutokana na chuki zake binafsi Hakimu huyo na udini uliyokithiri kwake. Mwanendo wa hukumu unaonesha na unatufanya Waislamu tuamini kuwa Hakimu Luhwago ni mdini na ametekeleza adhma yake hiyo kwa kutumia mamlaka aliyonayo.

Waislamu tunaamini kuwa Hakimu Luhwago ni kirusi cha udini kinachofanya katika chombo cha kusimamia sheria hivyo tunaiomba mamlaka husika kufuatilia jambo hili kwa haraka na kisha kumwajibisha muhusika ili Waislamu wa Tanzania waendelee kuwa na imani na chombo hiki cha kusimamia sheria ambacho ni sehemu ya muhimili wa Dola.

Kwa Waislamu wanamume kofia ni vazi la ibada na kitendo cha kumtaka Bw. Ally avue ni kumnyima haki yake ya kuabudu waislamu tumeipokea hukumu hii ya Luhwago kama maamuzi ya makusudi ya uchokozi dhidi ya ibada zetu.

Hukumu hii kwa Waislamu tunaifananisha na hukumu iliyotolewa Mkoani Morogoro dhidi ya Rajabu Dibagula ambayo nayo ulitaka kuvunja uhuru wa kuabudu wa Waislamu.

Waislamu wa Tanzania ingawaje bado tuna imani na Mahakama na Serikali kwa ujumla wake juu ya kutekeleza jambo hili limetuuma na tunaitaka mamlaka husika itoe ufafanuzi juu ya sheria, kama kuvaa kofia ya Kiislamu Mahakamani ni kosa kisheria.

Kwa upande wetu Waislamu tuaendelea kulifuatilia kisheria jambo hili na ikiwa ndani ya siku saba halijapatiwa ufumbuzi Waislamu tutatafuta njia mbadala ya haki hiyo. Mwisho tunawashukuru wanahabari kwa kutekeleza wajibu wao kwa kuijulisha jamii kuhusu uozo huu uliofanywa na mtendaji mbovu wa chombo cha kusimamia sheria.

Wabillah Tawfiq,



Alhaj Dr. Seif Sulle
MWENYEKITI KAMATI YA UMOJA VIJANA WA KIISLAMU
BAKWATA TAIFA

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...