Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, September 18, 2011

Mayweather amtwanga Ortiz KO raundi ya 4,na kutwaa ubingwa WBC




LAS VEGAS,Marekani

BONDIA Floyd Mayweather Jr.ameendelea kuwa bondia ambaye hajawahi kupigwa, baada ya kumsimamisha mpinzani wake, Victor Ortiz, katika pambano la kuwania ubingwa wa Welter lililofanyika usiku wa kuamkia jana mjini Las Vegas nchini Marekani. .

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Marekani AP, Mayweather aliibuka na ushindi huo, baada ya kumchapa Ortiz, dakika ya 2:59 ya raundi ya nne kwa kumshindilia makonde mfululizo yaliyomfanya mpinzani wake kwenda chini.



Kwa mujibu wa shirika hilo la habari, kisago hicho kilikuja baada ya mabondia hao kutoka mapumziko ambapo Ortiz alimfuata moja kwa moja Mayweather katikati ya ulingo na baada ya kugonganisha mikono, Mayweather aliachia konde la mkono wa kushoto na kufuatiwa na la mkono wa kulia ambayo yalimfanya Ortiz kuanguka chini.

AP ilieleza kuwa baada ya Ortiz kuanguka chini alijaribu kunyanyuka kwa shida lakini mwamuzi, Joe Cortez, akaamua kumaliza pambano.

“Tuligonganisha glove na tukawa tayari kupambana na baadaye nikaachia konde la mkono wa kushoto na kulia,” alisema Mayweather. “Ulingoni unapaswa kujilinda mwenyewe muda wote,”aliongeza bondia huyo.

Hata hivyo kabla ya pambano hilo kumalizika, raundi hiyo ilionekana kuwa tayari na utata, baada ya Ortiz,kumpiga kichwa makusudi Mayweather jambo ambalo lilimfanya aonywe na mwamuzi Cortez,lakini baada ya hapo Ortiz akaenda kumbusu Mayweather juu ya shavu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...