Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, February 8, 2012

RAIS JAKAYA NA MAKAMU WAKE WASHUHUDIA ZOEZI LA UTIAJI SAINI MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO WA KUDHIBITI MAHARAMIA (MoU) KATI YA TANZANIA, MSUMBIJI NA AFRI

Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal (nyuma) wakishuhudia zoezi la utiaji saini wakati Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Husein Mwinyi, akisaini mkataba wa makubaliano (MoU) ya Ushirikiano katika mapambano dhidi ya Maharamia kati ya Tanzania, Afrika ya Kusini na Msumbiji, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam, leo Februari 7, 2012. Kushoto ni Waziri wa Ulinzi wa Msumbiji, Filipe Jacinto Nyusi na (kulia) ni Waziri wa Ulinzi wa Afrika ya Kusni, Lindiwe Sisulu. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Rais Jakaya Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali wakishuhudia Waziri wa ulinzi wa Msumbiji Bw Filipe Jacinto Nyarusi (shoto)na wa Tanzania Dr Hussein Mwinyi wakibadilishana nyaraka huku wa Afrika Kusini DKT L.N. Sisulu akitazama baada ya mawaziri hao kutiliana saini ya mkataba wa makubaliano (moU) katika mapambano dhidi ya maharamia kati ya nchi zao.Picha/Ikulu

Rais Jakaya Kikwete akiongea baada ya mawaziri hao kutiliana saini ya mkataba wa makubaliano (moU) katika mapambano dhidi ya maharamia kati ya nchi zao.Picha/Ikulu

Rais Jakaya Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali wakiongea na Mawaziri wa ulinzi wa Msumbiji Bw Filipe Jacinto Nyarusi (shoto), wa Tanzania Dr Hussein Mwinyi (wa pili kushoto), na wa Afrika Kusini DKT L.N. Sisulu baada ya mawaziri hao kutiliana saini ya mkataba wa makubaliano (moU) katika mapambano dhidi ya maharamia kati ya nchi zao. Picha/Ikulu

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...