Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, March 13, 2012

Airtel Tanzania yazindua programu ya kuwawezesha wasichana shule za sekondari nchini.

Kumwelimisha mwanamke ni kuielimisha jamii nzima Airtel Kampuni ya simu za mikononi ya Airtel Tanzania kupitia kitengo cha huduma Kwa jamii imezindua programu ya uwezeshaji kwa wasichana itakayo wawezesha wasichana wenye umri kati ya miaka 14 mpaka 18 katika harakati za kufanikisha malengo yao ya baadae na kuwajengea uwezo wa kujiamini huku mafunzo hayo yakiwa yamebeba ujembe usemao “jenga maisha yako ya baadae”

Akiongea wakati wa ufunguzi wa Programu hiyo iliyofanyika shule ya sekondari ya wasichana Canossa iliyopo Tegeta jijini Dar-es-Salaam Meneja Huduma kwa jamii Bi Tunu Kavishe alisema “Programu yetu ina lenga kuwawezesha wasichana wote walioko shule za sekondari ikiwa ni muendelezo wa dhamira ‘Airtel Shule yetu’ ya kutoa elimu kwa jamii hasa wasichana ili kuendeleza mahusiano yetu mazuri kati ya kampuni na wateja wetu waaaminifu.

Mbali na hayo ni ukweli kwamba wasichana wanahitaji sana uelewa wa kutosha pamoja na kutimiza malengo ili kuendelea kufanya vizuri zaidi kitaifa au katika ramani ya dunia, Airtel inaamini wasichana hawa wanahitaji nafasi zaidi, mbali na masomo wanayosoma wanatakiwa kujifunza mbinu mpya za maendeleo kutoka kwa wasichana wenzao na wakubwa ambao wamewazidi umri pia.

Nae,Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Kampuni ya Airtel Bi.Adriana Lyamba ambae ndie aliyekuwa mtoa mada katika ufunguzi wa program hiyo kwa mara ya kwanza alisema “najisikia fahari sana kwa Airtel kunipa nafasi ya kuwa mtoa mada wa kwanza mara baada ya ufunguzi wa program
hii ya kuwawezesha wanawake wenzangu katika shule za sekondari ya wasichana ya Canossa.

Naiomba Airtel kuhakikisha programu hii itaendelea kwa shule nyingine za wasichana Tanzania na igusie mitaala mbali mbali ya uendelezaji wa taaluma kwa wasichana kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kujiamini na kufanya maamuzi sahihi katika maisha.tutawaomba wafanyakazi wengine wa
Airtel pamoja na wadau wetu katika biashara kujumuika nasi ili kuwaongezea na kuwapa wanafunzi uzoefu na mbinu mbalimbali kwa kufanya hivyo itawaweze kuelewa ni jinsi gani wataweza kuchagua na
kuendeleza taaaluma bora kwa maisha yao”.

“Kuna msemo unaosema kuwa ‘kumwelimisha mwanamke ni kuielimisha jamii nzima’ kwahiyo tunaamini elimu mtakayotoa sasa itakuwa chachu ya maendeleo kwa vizazi vijavyo” aliongeza Bi Adriana Tumejidhatiti kuisaidia jamii ya kitanzania,mbali na programu hii ya kuwawezesha wasichana tumekuwa tukisaidia sekta ya elimu kupitia programu ya Shule Yetu kwa kugawa vitabu katika shule za sekondari nchini na nia yetu ni kuendeleza kiwango cha elimu kwa kuwezesha upatikanaji wa vitabu kwa urahisi zaidi kwa wanafunzai wa shule ya sekondari.tangu tulipoanza hii programu ya kusadia vitabu katiaka shule ya sekondari kwa miaka saba iliyopita tumeweza kuwafikia zaidi ya sekondari 800 ambazo zipo nchi nzima.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...