Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, March 9, 2012

CHAMA CHA NGUMI ZA KULIPWA NCHINI CHATAMBULIKA KIMATAIFA

CHAMA
CHA NGUMI ZA KULIPWA NCHINI CHATAMBULIKA KIMATAIFA

Na Mwandishi
Wetu

SHIRIKISHO la Dunia la ngumi za kulipwa (WPBF) limempa hati ya kuwa
mwakilishi wa Shirikisho hilo nchini Rais wa Shirikisho la ngumi za kulipwa
nchini (TPBO).
Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari kwa mtandao na Rais
wa TPBO Yassin Abdala 'Ustadhi' ilisema kuwa Shirikisho hilo lenye makazi yake
nchini Marekani limempa hati hiyo ambayo itamruhusu kutoa taarifa muhimu za
jinsi mabondia wa ngumi za kulipwa wa Tanzania wanavyoingizwa katika viwango vya
Shirikisho hilo.
Alisema, sambamba na hilo pia litawasaidia mabondia
watanzania kuweza kupata nafasi ya kugombea mikanda ya Shirikisho hilo.
"Ni
jambo zuri kwa mabondia watanzania kwani watakuwa wanajua kila kitu kuhusu
viwango vyao kuingizwa katika Shirikisho hilo lakini pia kupata nafasi ya
kuwania mikanda hiyo ambayo itamsaidi kutambulika Ulimwenguni,"
alisema.
Sambamba na hilo pia Ustadhi amempongeza Mpiga picha wa Kampuni ya
Business Times Limited inayochapisha magazeti ya Majira, Spoti Starehe na
Business time,pamoja na Jarida la Maisha, ambaye pia ni Kocha wa Kimataifa wa
Mchezo wa Masumbwi, Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mchango wake katika kuhakikisha
anaukuza mchezo wa ngumi bila kubagua.
Alisema, Super D amekuwa ni msaada
mkubwa sana katika kila maandalizi ya mchezo kwa kuwasaidia waandaaji ambao
hupungukwa vifaa vinavyohusu mchezo hususan glovus na vifaa vingine.
Sambamba
na hilo amekuwa akifuatilia mapambano ya ngumi popote pale hata mkoani ,na huku
akiyaripoti yote yanayofanyika huko nje ya Dar es salaam kwa galama zake
mwenyewe.
"TPBO tunayo macho yenye kuona na kuthamini michango ya watu wa
aina yako hivyo tunakuahidi kukupatia cheti cha kuthamini mchango wako katika
tasnia hii ya mchezo wa ngumi katika wakati muafaka," alisema.
Aliongeza
kuwa yapo mengi ya kumshukuru kwani pia ameakuwa akiwasaidia mabondia wa mikoani
kwa kuwauzia vifaa vya mchezo kwa bei ndogo kuliko hata ile ya madukani , hivyo
kuwawezesha mabondia hao kuwa na uwezo wa kumiliki vifaa vya ngumi kiurahisi

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...