Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, May 18, 2012

FFU ! wa Ngoma Africa kuvaana na Wakameruni 5,000 Stuttgart,Ujerumani


Wakameruni wapatao zaidi ya 5,000 waishio nchini ujerumani wanatalajia kujimwaga na muziki wa dansi wa Ngoma Africa Band huko mjini Stuttgart,Ujerumani siku ya jumamosi
20 Mai 2012,katika sherehe maalumu kwa ajili  ya nchi yao "Cameroni Challenge" .
Kamati ya maandalizi ya jumuia ya wakameruni nchini Ujerumani imetoa mwaliko kwa
bendi maarufu ya muziki wa dansi barani Ulaya Ngoma Africa band almaarufu FFU,kutumbuiza
katika sherehe hizo zitakazo fanyika mjini Stuttgart,nchini Ujerumani,ambako zitahudhuriwa na
wakameruni 5000 pamoja na wageni wa mataifa mbali mbali.
Mzimu huo wa dansi Ngoma Africa band aka FFU unatarajiwa kutoa burudani ya kuwapandisha
mzuka wadau wote watakao jimwaga uwanjani,
Ngoma Africa band sasa wanatamba na mpini wao mpya " Uhuru wa Habari" sikiliza hapa www.ngoma-africa.com au http://www.ngoma-africa.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...