Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, May 18, 2012

WENGI WAJITOKEZA KUUAGA MWILI WA ALIYEKUWA MCHEZAJI WA SIMBA, MAREHEMU PATRICK MAFISANGO


 Wachezaji wa timu ya soka ya Taifa (Taifa Stars), wakiwa wamebeba mwili wa aliyekuwa mchezaji wa timu ya Simba, marehemu Patrick Mafisango, tayari kutolewa heshima za mwisho leo kwenye viwanja vya TCC Chang'ombe, Dar es Salaam.
 Msafara wa mwili wa Mafisango ukiongozwa na Trafiki, kuingia viwanja vya TCC Chang'ombe, Dar es Salaam leo

 Baadhi ya watu waliojitokeza kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Mafisango, wakiwa wamejipanga tayari kkupokea kwenye viwanja vya TCC Chang'ombe.
                                    Mmoja wa ndugu wa karibu wa marehemu Mafisango, akilia kwa uchungu

 Mchezaji wa Simba na Taifa Stars, Mwinyi Kazimoto akifarijiwa
                      Jamaa wakimfariji mlinda mlango wa Simba, Juma Kaseja aliyekuwa akilia kwa uchungu
                           Mwombolezaji akiwa ameshika bango la kumuombe dua marehemu Mafisango
 Mchungaji akiendesha ibada maalumu ya kuuaga mwili wa marehemu Mafisango
 Katibu Mkuu wa Yanga, Mwesiga Selestine akitoa salamu za Yanga wakati wa kuugana mwili wa Mafisango
 Askari wakilinda usalama
 Mwanachama maarufu wa Simba, Philemon Sarungi akimfariji Mwenyekiti wa Simba , Aden Rage ambaye alishindwa kuendelea kusoma risala na kuangua kilio.
 Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah akisoma salamu za rambirambi za shirikisho hilo
 Mwili wa marehemu Mafisango
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangala akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Mafisango
 Viongozi wa michezo wakitoa heshima za mwisho
 Baadhi ya wachezaji wakiwa kwenye foleni tayari kutoa heshima za mwisho
 Wananchi wakiwa wamejipanga kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Mafisango
                                                         Ni Kilio kila mahala


 Nurdin Bakari akimfariji Kazimoto
Sehemu ya umati wa waombolezaji waliofika kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa  marehemu Mafisano. Picha na Dotto Mwaibale

1 comment:

  1. daa simba tumepoteza kifaa, pole kwa wadau wote,REST IN PEACE MAFISANGO.

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...