Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, May 16, 2012

Rais Kikwete atembelea Ofisi za Tume ya Kuratibu Maoni ya Katiba jijini Dar es Salaam


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jana alitembelea ofisi za Tume ya kukusanya na kuratibu maoni juu ya katiba zilizopo katika jengo jipya katika Wizara ya Mambo ndani jijini Dar es Salaam.Akizungumza na wajumbe wa Tume hiyo Rais Kikwete alirudia ahadi yake ya kuwapatia nyenzo za kazi ikiwemo usafiri ili kuiwezesha tume hiyo kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.Pichani Rais akizungumza na wajumbe wa tume hiyo katika ukumbi wa mikutano uliopo katika jengo la tume hiyo jana.
Mwenyekiti wa Tume ya Kuratibu maoni juu ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba(kulia) akizungumza na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati Rais alipomtembelea ofisi kwake jana.Wengine katika picha ni Makamu mwenyekiti wa tume hiyo Jaji mkuu Mstaafu Mhe. Agostino Ramadhani(Watatu kushoto),Waziri wa Katiba na SheriaMhe. Mathias Chikawe(Wapili kushoto) na kushoto ni naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Angela Kairuki.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo naProfesa Mwesiga Baregu ambaye ni mjumbe  wa Tume ya kuratibu maoni kuhusu katiba wakati Rais alipotembelea ofisi za tume hiyo jijini Dar es Salaam jana(picha na Freddy Maro).
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(Wanne kushoto Mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Tume ya kuratibu maoni  ya Katiba wakati alipotembelea ofisi za tume hiyo Jijini Dar Es Salaam jana.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...