Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, October 6, 2013

KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI OMBENI SEFUE ATEMBELEA OFISI ZA WAKALA YA SERIKALI MTANDAO LEO JIJINI DAR ES SALAAM.


Picha na 1Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (katikati) akiwasili katika ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao zilizopo jengo la TTCL mtaa wa Samora leo jijini Dar es salaam kwa lengo la kuangalia shughuli za usimamizi wa mifumo na matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika uendeshaji wa shughuli za serikali.  Picha na 2Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea na viongozi wa Wakala ya Serikali Mtandao na waandishi wa habari  leo jijini Dar es salaam mara baada ya kupokea taarifa  kuhusu maendeleo ya Tovuti Kuu mpya ya serikali inayosimamiwa na Wakala ya Serikali Mtandao chini ya Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma. Balozi Sefue amefafanua kuwa Tovuti Kuu ya Serikali iliyoanzishwa itawawezesha wananchi kupata taarifa na huduma mbalimbali zinazotolewa na serikali.  Picha na 3Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Jabiri Bakari akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mpango wa serikali katika kuhamasisha na kuendeleza matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika shughuli za serikali  kupitia Tovuti Kuu mpya ya serikali iliyoanzishwa  kwa lengo la kuboresha na kurahisisha utoaji wa taarifa na huduma kwa umma, kuhamasisha ushirikishwaji wa raia katika utoaji wa maamuzi yanayowahusu na kuwezesha uwepo wa serikali iliyo wazi.
Picha na 4Baadhi ya viongozi wa Wakala ya Serikali Mtandao iliyo chini ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na waandishi wa habari wakiwa katika mkutano na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue. Picha na 5Picha na 5. Mwonekano mpya wa Tovuti Kuu ya Serikali ambayo inapatikana katika anuani ya  www.egov.go.tz. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
……………………………………………………………………………….
NA   MAGRETH   KINABO- MAELEZO
SERIKALI YASEMA TEHAMA KUFIKA HADI VIJIJINI
 SERIKALI imesema kwamba   inatarajia kuboresha   Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kila kijiji ili  huduma zake ziweze kuwa karibu na wananchi, hatua  hiyo  itasaidia kuwapunguzia gharama wanazozitumia.
 
Aidha  Serikali  imeeleza  kwamba iteendelea kujenga uwezo wa  kiufundi wa   kuweza kuzuia  uvujaji wa siri, uhalifu na udhibiti wa sheria ndani ya  vyombo vyake ili taarifa za siri zisiweze kuvuja.
 
 Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi  Ombeni Sefue  wakati alipotembelea  ofisi ya  Wakala  ya Serikali Mtandao(e GA) jijini Dares Salaam kwa ajili ya kuzungumza na menejimenti na wafanyakazi.
 
“Leo nimetembelea ofisi hii. Ni eneo la kipaumbele kwa Serikali   kwa kuongeza matumizi   ya TEHAMA kwa Serikali, tija, kasi ya utendaji kazi na huduma za Serikali. Hivyo sehemu hii ni muhimu ya kuifanya Serikali iwe karibu na wananchi. Tovuti hii iwe ni dirisha   la mwananchi kutatuliwa shida yake.,”alisema huku akitoa wito kwa wananchi wawe tayari kuitumia.
 
 Balozi Sefue  alisema tatizo la changamoto  la TEHAMA   kuhusu  uvujaji wa siri  lipo dunia nzima hata Marekani  wanakabiliana  nalo ,hivyo  ufumbuzi wake si kuachana nalo bali kuzuia uvujaji huo na uhalifu kwa kujenga uwezo wa udhibiti.
 
“Lazima kuwe na udhibiti mfano wa kisheria  tayari tunayo sheria  tutaendelea kuiboresha kulingana na changamaoto zitakazo kuja,” alisisitiza Balozi Sefue.
 
 Alisema kupitia TEHAMA wananchi wataweza kupata matibabu au elimu  na kulizia huduma wanazotakiwa kuzipta mfano miradi ya visima vya maji imefikia hatua  zipi.
 
Aliongeza kuwa hivi sasa wakala huo unaandaa mifumo ya kuwezesha Wizara, Idara na taasisi mbalimbali za Serikali kufanya kazi kwa ushirikiano.
 
Akizungumzia  kuhusu ufikishaji wa huduma katika maeneo ya vijijini, Mtendaji Mkuu wa (eGA) Dk. Jabiri Bakari alisema watatumia ubunifu ili kuhakikisha huduma ya TEHAMA inatumika kwenye maeneo hayo mfano kwa kutumia sehemu za mkononi  za kawaida.
 
 Wakala hiyo  ulianzishwa Julai mwaka 2012, ambapo taarifa mbalimbali za Serikali kutoka Wizara, Idara  , wakala na taasisi zake zitapatikana kupitia mtandao  wa wakala hiyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...