Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, October 6, 2013

KLITSCHKO AMSHINDA POVETKIN KWA POINTI, PAMBANO LAO LILIJAA KUKUMBATIANA SANA


Wladimir Klitschko amefanikiwa kumshinda Alexander Povetkin kwa pointi baada ya kucheza kwa raundi 12.

Hata hivyo, pambano hilo halikuwa zuri sana kutokana na mabondia hao kutumia muda mwingi wakikumbatiana.
Ilionekana Klitschko alisoma uchezaji wa Mrusi huyo na zaidi alikuwa anahofia ukali wa ngumi zake za kushtukiza, hivyo akatumia muda mwingi akimkumbatia.
Pamoja na kukumbatia Klitschko alikuwa akipiga ngumi za kushtukiza ambazo zilionekana kumwelemea Povetkin na mara nne alishindwa kujizuia na kulamba sakafu.
Hata hivyo, baada alilalamika kwamba aliangushwa mara mbili tu na zilizobaki alisukumwa mpinzani wake Klitschko ambaye alimshinda kwa pointi 119-104.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...