Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, October 10, 2013

Mbeya City yazidi kupepea, Azam, Mtibwa Sugar wazindukaMbeya City

WAKATI Azam ikizinduka na kuondoka na 'mdudu' wa sare baada ya kuitungua Mgambo JKT mabao 2-0, wageni wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Mbeya City ya jijini Mbeya imeendelea kutakata baada ya kuisasambua Rhino Rangers nyumbani kwao mjini Tabora kwa kuilaza mabao 3-1.

Ushindi wa timu hizo mbili zimezifanya ziisogelee Simba kwa kufikisha pointi 14, moja pungufu na zile ilizonazo vinara hao ambao leo hawakushuka dimbani.
Azam ilipata ushindi huo kwenye uwanja wa Chamazi na shukrani zikienda kwa kinda Faridi Mussa Maliki na Kipre Tchetche na kuipeleka Azam hadi nafasi ya pili mbele ya Mbeya City wakizidi kwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Katika mechi nyingine, Ruvu Shooting imetoshana nguvu dhidi ya maafande wenzao wa Oljoro JKT baada ya kutoka sare ya mabao 2-2, mabao ya timu hizo yakifungwa na Elias Maguri wa Ruvu na Fikiri Mohammed wa Oljoro waliyofunga kila mmoja mawili.
Nao mabingwa wa zamani wa Tanzania, Mtibwa Sugar imezinduka nyumbani kwao Manungu Morogoro baada ya kuwatungua JKT Ruvu mabao 2-1 na kujivuta hadi nafasi ya tisa.
Mabao mawili ya Juma Luizio yalitosha kuibeba Mtibwa ambao mwishoni mwa wiki walinyanyaswa na Yanga kwa kulazwa mabao 2-0, na mkongwe Salum Machaku akiifungia JKT bao pekee la kufutia machozi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...