Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, October 10, 2013

PSPF yawaomba wasanii, wanamichezo kujiunga na Mpango wa Uchangiaji wa Hiari





Nilipopokea mwaliko kutoka Mfuko wa Pensheni (PSPF) ukiniomba kuhudhuria kwenye hafla fupi ya chakula cha mchana pamoja na wadau wa tasnia ya sanaa na michezo nchini, sikuelewa mara moja lengo la hafla hiyo lakini baada ya kufika ukumbini na kupata ufafanuzi wa mabadiliko makubwa yaliyofanywa na PSPF nikapata somo.

Kumbe PSPF sasa si kwa watumishi wa umma pekee bali hata wanamuziki, waigizaji, wachezaji na hata watu wengine waliokwenye sekta zisizo rasmi wanaweza kujiunga na kufaidika na mafao yanayotolewa na mfuko huo.

Wadau wengi wa tasnia ya sanaa na michezo walijitokeza kwenye halfa hiyo tukianza na Elizabeth Michael Lulu, Mwanamitindo mwenye mafanikio makubwa ndani na nje ya nchi, Flaviana Matata, Mtitu, Steve Nyerere, Nahodha wa timu ya taifa ya soka wanawake Sophia Mwasikili na wadau wengine wengii...

Elizabeth Michael (Lulu) na Flaviana Matata
Steve Nyerere

Meneja wa Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF, Costantina Martin

Meneja wa Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF, Costantina Martin anasema lengo kukukutana na wadau hawa ni kutambulisha kwao mpango wa uchangiaji wa hiari (PSPF SUPPLIMENTARY SCHEME-PSS) ambao unamwezesha mtu yeyote kujiunga na mpango huo awe ameajiriwa au amejiajiri mwenyewe.

“Uzuri wa mpango huu wa uchangiaji wa hiari, unaruhusu hata wanachama waliokwenye mifuko mingine kujiunga nao lakini pia mwanachama anayohiari ya kuhamia kwenye mpango wa uchangiaji kwa mujibu wa sheria yaani Main Scheme” Anasema Costantina

Anasema kuwa kiasi cha michango kwenye mpango wa hiari kinaanzia shilingi elfu kumi (10,000) kwa mwezi na hakuna kiwango cha juu ambapo mwanachama yuko huru kuchagua kuwasilisha michango kwa wiki, mwezi au kwa msimu na michango hiyo inawasilishwa kupitia akaunti ya benki, au wakala wa malipo wa M-Pesa na Airtel Money.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...