Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, October 10, 2013

Zaidi ya Benki 7 zaungana na Airtel kuwezesha wateja kuhamisha pesa kutoka akaunti zao za benki kwenda kwenye akaunti ya Airtel money masaa 24 siku 7 za wiki.


Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel, Beatrice Singano Mallya
Ni njia salama, rahisi ya kupata pesa kupitia kutoka Airtel

Airtel Tanzania kupitia huduma yake ya Airtel money imeanzisha ushirikiano na benki mbalimbali nchini na kuwawezesha wateja wake kuhamisha pesa kutoka kwenye benki akaunti zao na kuziweka kwenye akaunti ya Airtel money

Benki ambazo zimeingia katika ushirikiano huo na Airtel ni pamoja na Tanzania Postal Bank, Bank of Africa, Kenya Commercial Bank, Barclays Bank, Akiba Commercial Bank, Exim Bank, Amana Bank, Mkombozi Commercial Bank na Standard Chartered bank.

Ili kupata orodha ya huduma za benki husika mteja anatakiwa kupiga namba zifuatazo na kufuata maelezo Tanzania Postal Bank -*150*21#, Bank of Africa -*150*13#, Kenya Commercial Bank -*150*22#, Barclays Bank -*150*20#, Akiba Commercial Bank *150*10#, Exim Bank -*150*11#, Amana Bank -*150*12#, Mkombozi Commercial Bank -*150*06# , Standard Chartered Bank - *150*65#

Akiongea juu ya ushirikiano huo Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel bi Beatrice Singano Mallya alisema" kuanzishwa kwa mpango huu wa huduma ya Airtel money na za kibenki kutawawezesha wateja Airtel kutoa pesa kwenye akaunti zao za benki na kuziweka kwenye simu zao yani akaunti ya Airtel money kirahisi bila kutembelea ofisi za benki.  Huduma ya Airtel Money ni suluhisho la huduma za kifedha ikiwa na zaidi ya mawakala 20,000 , kupitia mtandao wetu mpana ulioeneea nchi nzima tunauhakika wa kuwafikia watu wengi zaidi hasa wa maeneo ya vijijini"

Tunaamini ushirikiano na benki zingine kutaendelea kuwaletea wateja wa huduma ya Airtel money ufanisi na urahisi wa upatikanaji wa fedha kutoka kwenye benki zao wakati wote mahali popote nchi nzima."

Mallya aliendelea kusema Airtel imedhamiria kutoa huduma za kiubunifu na gharama nafuu kwa watanzania kwani tunatambua tecknolojia ya simu inazidi kukua ikiunganisha watu na kubadili maisha ya jamii zetu.

Huduma ya Airtel money pia inawezesha makampuni, watoaji huduma za kitechnologia na makundi mbali mbali kufanya malipo na kukuza huduma za kifedha nchini. "Airtel imejipanga kutoa huduma zitakazoongeza urahisi na ufanisi katika maisha ya kilasiku kwa mtanzania" aliongeza Mallya.

Akiongea kuhusu ushirikiano meneja huduma wa Airtel Money Bw , Asupya Nalingingwa Alisema "tunafuraha kuingia kwenye makubaliano haya ya ushirikiano wa kutoa huduma za kifedha na benki hizi tofauti ambapo kwetu ni nafasi nzuri ya kuendelea kuboresha huduma za kifedha nchini na kuwafikia wateja wa benk hizi na wateja wa Airtel wasio na huduma ya benki hizo maeneo ya karibu."

Huduma ya Airtel money inawawezesha wateja kulipia bili zao, kutuma na kupokea pesa na kufanya miamala mbalimbali, huduma hii inapatikana kwa wateja wa malipo ya awali na ya baada , kujiunga na huduma hii ni bure kwa kupita maduka ya Airtel na mawakala nchi nzima. Airtel inatoa huduma ya Airtel money kwa msharika na watu binafsi kama njia mbadala ya malipo.

Airtel pia kupitia Airtel Money kwa sasa imezindua promosheni mpya ya Hakatwi mtu hapa  inayowawezesha wateja wa Airtel kutuma na kupokea pesa bila makato yoyote popote pale nchini.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...