Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, October 5, 2013

SHULE YA WAMA - NAKAYAMA WAPEWA VIFAA VYA MICHEZO


 Mkurugenzi  Mtendaji  wa Kampuni ya Montage Tanzania,Teddy  Mapunda  wa tatu kutoka (kulia) akimkabidhi  mpira Mwanafunzi wa  kidato cha kwanza  wa Shule ya  Sekondari ya  wasichana  ya  WAMA  - Nakayama iliyopo Rufiji, mkoani Pwani  Rehema   Mshama(kulia)  ikiwa ni mchango wake katikakuwasaidia watoto yatima  na wanaoishi katika mazingira  hatarishi  ili  waweze kujiendeleza katika sekta ya michezo. Makabidhiano hayo yalifanyika jana kwenye ofisi ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), jijini Dares Salaam.
 Mkurugenzi  Mtendaji  wa Kampuni ya Montage Tanzania, Teddy  Mapunda  wa nne kutoka (kushoto ) akimkabidhi  mpira  Mwalimu wa   Michezo wa  Shule ya Sekondari ya WAMA-  Nakayama iliyopo Rufiji, Mbwana  R. Mbwana  wa tatu kutoka (kulia) ikiwa ni mchango wak katika  kuwasaidia watoto  yatima  na  wanaoishi katika mazingira hatarishi  ili waweze kujiendeleza  katika sekta ya michezo. Makabidhiano hayo yalifanyika jana kwenye ofisi ya Taasisi ya Wanawake na  Maendeleo (WAMA), jijini Dares Salaam.
Mwalimu wa   Michezo wa  Shule ya Sekondari ya Wama   Nakayama iliyopo Rufiji, Mbwana  R. Mbwana   wa tatu kutoka (kulia)  na wanafunzi wa shule hiyo  wakifurahia  vifaa vya michezo  baada    wa  Mkurugenzi  Mtendaji  wa Kampuni ya Montage Tanzania, Teddy  Mapunda   kutoa  mchango  huo  ili  kuwasaidia watoto yatima  na  wanaoishi katika mazingira  hatarishi katika sekta ya michezo. Makabidhiano hayo yalifanyika leo kwenye ofisi ya Taasisi ya  Wanawake na Maendeleo (WAMA), jijini Dares Salaam. Picha zote na Magreth Kinabo -maelezo.
****************************************
Na Anna Nkinda – Maelezo
Wadau wa michezo, wapenzi wa amani,  afya na maendeleo ya vijana  nchini wameshauriwa kuwekeza zaidi katika michezo kwani inafaida kubwa katika maisha ya mtoto kwa kuwa  inamuepusha na vishawishi vingi vya afya ya uzazi.
 Ushauri huo umetolewa leo na Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Daud Nasib wakati akiishukuru Kampuni ya Montage Tanzania kwa kutoa vifaa vya michezo kwa ajili ya shule ya Sekondari ya   wasichana ya WAMA- Nakayama iliyopo Rufiji mkoani Pwani.
Nasibu alisema kama wadau hao watahitaji kupata msaada wa kuzitambua shule zenye mahitajia maalum  kama ya WAMA- Nakayama watawasaidia  kuzitambua shule hizo.
Alisema mchango huo ni mzuri kwani unahamasisha umuhimu wa michezo shuleni  kwa kuwa michezo ni muhimu kwa afya ya akili na humuwezesha kijana kukua  vizuri na kwa usalama pale atakapokuwa  mwanamichezo kutamsaidia  kujiepusha na mambo mengi yanayoweza kumletea tabu katika maisha yake.
Akiongea mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo vya michezo Teddy Mapunda ambaye niMkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo alisema wametekeleza yale ambayo waliyaahidi walipotembelea shule hiyo wakati wa sherehe za sikuku ya Eid Mubarak alisikia watoto wanapenda kushiriki katika michezo lakini kulikuwa na upungufu wa vifaa vya michezo na kuamua kuwasaidia vifaa hivyo.
Teddy aliwaomba wanafunzi hao kutumia vipindi vya michezo kucheza kwa bidii kwani michezo ni ajira, uhai na inaongeza akili shuleni pia inaleta amani na kujenga urafiki na ushirikiano.
Kwa upande wake Mwalimu wa michezo wa shule hiyo Mbwana R. Mbwana alishukuru kwa jezi na mipira waliyopewa kwa nia ya kuendeleza michezo shuleni hapo kwani itawasaidia kushiriki michezo mbalimbali katika ngazi ya shule na UMISETA.wanakabiliwa na ukosefu wa vuafaa vya michezo shuleni hapo.
Mwalimu Mbwana alisema mwaka juzi katika mashindano ya UMISETA walipeleka wanafunzi saba katika ngazi ya mkoa huko kibaha na mwaka jana walipeleka wawili  ila kupatikana kwa vifaa hivyo anaamini miaka ijayo watapeleka wanafunzi wengi zaidi  na kufanya vizuri zaidi.
Kampuni ya Montage Tanzania imetoa msaada wa mipira ya kuchezea mpira wa miguu mitano na pete minne, jezi za mpira wa pete 18 na mpira wa miguu 26 na jezi za mlinda mlango wa mpira wa miguu mbili.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...