Afisa wa Usalama (mwenye suti) akiangalia usalama katika moja la
lango ya kuingia kwenye Uwanja wa Taifa.
Viongozi wa Azam TV wakiteta jambo na Ofisa Habari
wa TFF, Boniface Wambura baada ya kuzuiwa kurusha live mchezo huo.
UONGOZI wa klabu ya Yanga umewatimua wapiga picha
wa Azam TV kabla ya mpira kuanza wakiwakataza wasirushe mchezo wao dhidi ya Mtibwa
Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga walikataa kurusha mchezo huo kwa madai kuwa
mazungumzo yao kati ya klabu yao na Azam TV na Waziri wa Habari Utamaduni na
Michezo.
Lakini baada ya kufanyika kwa mazungumzo kati ya
pande hizo mbili wapiga picha wa Azam walionekana kurudisha kamera zao uwanjani
tayari kwa kurusha katika kipindi cha mchezo huo.
Hadi mapumziko tayari Yanga walikuwa wanaongoza kwa mabao
2-0, yaliyofungwa na Mrisho Ngassa dakika ya 6 na Didier Kavumbagu dakika ya
24.
Wafanyakazi wa Azam TV wakishangaa bila kujua la
kufanya
Didier Kavumbagu akiifungia Yanga bao la pili huku kipa wa Mtibwa, Hussein Sharrif akijitahidi kuokoa bila mafanikio
Mrisho Ngassa akishangilia bao lake la kwanza kuifungia Yanga toka ajiunga na timu hiyo kwa mara ya pili
No comments:
Post a Comment