Marquee
tangazo
Friday, April 22, 2011
DAVID HAYE AJIGAMBA KUMTWANGA WLADIMIR KLITSCHKO
DAVID Haye anapamba kuweka utaratibu wa mazoezi kwa ajili ya pambano lake dhidi ya Wladimir Klitschko na kisha atafanya hivyo pia kwa Vitali kabl ya kuamua kustaafu.
Bingwa wa Dunia wa WBA, Haye atatwangana na bingwa wa mataji ya IBF na WBO, Wladimir katika mechi ya kuunganisha mataji itakayochezwa Hamburg Julai 2 mechi ambayo inatarajiwa kutengeneza pauni milioni 40.
Haye hatimaye amesaini mkataba juzi baada ya miezi ya kufanya makubaliano ambapo kambi ya Haye ilikuwa golini kutaka liwepo pambano hilo.
Mpiganaji wa London amethibitisha kuwana anataka kuwepo kwa pambano hilo bila ya kujalia atalipwa kiasi gani na waandaaji wa mechi wamefuata matakwa ya Klitschko mwenye umri wa miaka 35.
Haye mwenye umri wa miaka 30 alisema: "Nitaweka kipeperushi cha Maisha ya Wlad katika gym yangu ili kwamba kila wakati nitakapokuwa nikipigabag,padi au kupigana kwa mazoezi, itakuwa kichwani mwangu kwamba niko tayari kumuumiza.
"Nilishawahi kuweka vipeperushi ya wapinzani wangu wengine kabla ya kucheza mapambano yangu makubwa.
"Inanipa ari kwa kuziangalia huku nikiweza kufikiri kuhusu ngumi zangu za nguvu zikiwaangamiza. Klitschko atakuwa akiota analala katika barafu na ya kumshinda.
"Ni kitu kizuri kusaini baada ya kupita muda mrefu bila ya kitu chochote kutokea. Kisha kambi ya Klitschko iliwasilianana sisi na pambano limerejea.
"Sikujali ni wapi pambano litafanyika kwakuwa kutama kuwa na tokeo moja tu, kama litafanyika uani mwa nyumba yake au mbele ya chumba atapigwa kwa mtindo mmoja.
"Kila mmoja anajua sina mpango wa kupigana nikiwa na umri wa miaka 31 na kwamba bethidei yangu inakuja Oktoba.
"Lakini ninatumaini kuwa baada ya kupiga Wladimir, kaka yake Vitali ambaye ana umri wa miaka 39, atataka kujaribu kulipa kisasi kwangu kutokana na kumchakaza mdogo wake .
"Vitali naye atapita njia hiyo hiyo, mzee huyo atapoteza ubingwa wake wa WBC kwa kupigwa kama mdogo wake."
Haye amekubalia kugawana pesa 50-50 ingawa atakusanya sehemu kubwa ya mapato.
Pia ameruhuhusu kituo vya televisheni cha RTL cha Ujerumini akinachotumiwa na Klitschko, badala ya ARD ambacho kilikuwa kikirusha baadhi ya mechi zake.
Akina Klitschko pia wameweka sharti kuhusu kutengeneza ngovu na kutaka kuwepo daktari wa kijerumini kwenye kona yao.
Haye alisema: "Nitakwenda kupigana nyumbani kwake na hainiogopeshi hata kidogo. Nilishawahi kufanya hivyo na nitafanya tena.
"Niliunganisha mataji katika uzani wa cruiser kwa kumtwanga nyumbani kwake Jean-Marc Mormeck akiwa Paris, Nilitwaa ubingwa wa Dunia wa uzito wa juu kwa kutwanga, Nikolai Valuev mjini Nuremberg.
"Akitokea Klitschko yeyote anayetaka kupigana nimekubali, glovu zozote anazotaka, ni sawa kwangu... kuingia ulingoni akiwa wa pili, haijalishi kwangu.
Alisema masharti hayo watu hawatayafikiri wakati akimtwanga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment