Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, April 21, 2011

*TAASISI ZILIZOPIGA HATUA ZAOMBWA KUISAIDIA TANZANIA


Na Anna Nkinda – Arizona


Taasisi zilizoendelea ambazo zinashughulika na mambo ya afya zimeombwa kuisaidia Tanzania katika masuala ya elimu, wataalamu wa fani ya tiba na vifaa vya afya ili nchi iweze kukabiliana na tatizo la baadhi ya vifo vinavyotokana na upungufu wa madaktari bingwa pamoja na vitendea kazi .


Ombi hilo limetolewa leo (jana) na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea na wafanyakazi pamoja na wanafunzi wa Chuo kikuu cha AT Still upande wa shule ya afya ya meno na kinywa kilichopo Arizona nchini Marekani


Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema kuwa nchi ya Tanzania inakabiliwa na tatizo la upungufu wa wafanyakazi katika sekta ya afya pamoja na upungufu wa vifaa katika hospitali na vituo vya afya jambo ambalo linapelekea vifo vya baadhi ya wagonjwa wakiwemo kina mama wajawazito na watoto.


"Hivi sasa vifo vya kina mama wajawazito na watoto vimepungua, lakini bado tatizo lipo hii ni kutokana na upungufu wa vitendea kazi na wataalam mbalimbali wa Afya lakini kama mtatusaidia kutupatia ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa Tanzania ili waje kusoma katika chuo hiki hakika nchi itapata wataalamu wa kutosha na tatizo la madaktari bingwa litapungua kwa siku za usoni", alisema Mama Kikwete.


Kwa upande wake Dean of Student wa shule hiyo Jack Dillenberg alisema kuwa hivi sasa wanaangalia uwezekano wa kutoa ufadhili kwa wanafunzi mbalimbali hasa katika nchi zinazoendelea ila kitu wanachokifanya hivi sasa ni kutoa mikopo ambayo wanafunzi wanailipa taratibu mara baada ya kumaliza chuo na kupata ajira.


Dillenberg alisema,"Tutaangalia ni jinsi gani tunaweza kuwasaidia katika suala la kutoa ufadhili pamoja na madaktari bingwa ili kuweza kutatua tatizo la vifo vinavyotokana na ukosefu wa wataalamu wa fani mbalimbali za afya kwani kama vijana watasoma na kujikita zaidi katika fani ya afya hakika tatizo lililopo hivi sasa litapungua".


Mama Kikwete yuko Arizona kwa mualiko maalum uliotolewa na Project C.U.R.E ambao wameona jitihada zake za kupambana na kuhakikisha kuwa vifo vya watoto wachanga na kina mama wajawazito vinapungua na hivyo kuamua kufanya harambee ya kuchangia vifaa tiba kwa ajili ya hospitali, vituo vya afya na zahanati hapa nchini.




Mwenyekiti wa Taasisisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete, akimpatia zawadi Dean wa Chuo Kikuu cha AT STILL upande wa Shule ya afya ya meno na kinywa (Arizona School Of Dentistry and Oral Health kutoka A.T.Still University) huko Marekani Jack Dillenberg, baada ya kutembele chuo hicho na kujionea shughuli mbalimbali shuleni hapo jana Wapili kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mwanaidi Sinare Maajar. Picha Zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini Tanzania (WAMA) Mama Salma Kikwete (wapili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Dean wa Arizona School of Dentistry and Oral Health Jack Dillenberg, kuhusu umuhimu wa matumizi yakufundishia kifaa cha komputa alipotembelea na kuangalia jinsi ya mafunzo mbalimbali ya tiba ya meno na kinywa.


Mama Salma, akitembelea ghala la vifaa vya hospitali vya project ya C.U.R.E. huko Phoenix Marekani jana.
http://sufianimafoto.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...