MABONDIA wa ngumi za ridhaa wa mkoa wa Ilala wanatarajia kupanda ulingoni kesho katika ukumbi wa Panandipanandi, Ilala Dar es Salaam. ambapo kutakuwa na ngumi kutoka kwa mabondia mbalimbali toka pande zote za mkoa wa DAr es Salaam
Tamasha hilo litakalokuwa likitimua vumbi kila wiki inatarajia kuwakutanisha mabondia wa Ilala na wa sehemu nyingine za Dar es Salaam ili kuweza kujipima nguvu katika kuinua mchezo huo katika mkoa huo.
Katika Tamasha hilo kesho bondia Mbwana Matumla anayejiaandaa kwa ajili ya kushiriki katika kuwania ubingwa wa UBO pambano linalotarajia kufanyika siku ya Mei mosi katika ukumbi wa PTA dhidi ya Mkenya Gabriel Ochieng atachuana na mabonmdia Yohana Robert na Issa Sewa.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Mratibu wa Tamasha hilo kupitia Taasisi ya Kinyogoli foundation, Habibu Kinyogoli alisema mapambano yote yatakuwa katika raundi nne huku pambano la Mbwana likiwa katika uzito wa Kg 55 likiwa ni sehemu ya maandalizi ya pambano lake hilo.
Alisema, mkakati huo wa kuanzisha Tamasha akishirikiana na kocha msaidizi wa timu ya mkoa huo Rajabu Mhamila 'Super D' utasaidia kuinua vipaji vipya vya mchezo huo kwa kiasi kikubwa kwani kutawajenga wachezaji kujikita katika mchezo huo na kuufanya kama ndio ajira yao.
Alisema, katika kulifanikisha hilo anawaomba wadau mbalimbali kuwasaidia kuwadhamini ili waweze kufikia malengo yao katika kuinua vipaji hivyo.pia alisema kutakuwa na wageni waalikwa ambao watatoa mada mbalimbali kuhusu kuinua mchezo wa ngumi Tanzania akiwemo mdau wa ngumi.Innocente Melleck na mwingine Benedictor Hulilo ambao watakuwa wageni waalikwa
No comments:
Post a Comment