Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, April 24, 2011

VODACOM SHUFFLE DANCE…!!!

Pichani Juu na Chini ni Helkopta ikipita kandokando ya Bahari ya Hindi eneo la Ufukwe wa Sunrise Resort, wakati wa Tamasha la Vodacom la ‘Shuffle Dance’, lililoandaliwa maalum na kampuni hiyo kwa ajili ya kuweka na kuvunja rekodi ya dunia katika kitabu cha Matukio makubwa Duniani ‘Guinness Book Records’.Tamasha hilo lilifanyika kwenye Ufukwe wa Hotel ya Sunrise Kigamboni Dar es Salaam.

Muongozaji wa zoezi hilo akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Tamasha hilo.

Wasanii mbalimbali na vijana waliojitokeza kushiriki Tamasha la Vodacom ‘Shuffle Dance’, wakicheza staili moja kwa pamoja wakati wa Tamasha hilo lililofanyika kwenye Ufukwe wa Hoteli ya Sunrise Kigamboni Dar es Salaam, likiwa na lengo la kuvunja na kuweka rekodi ya Dunia katika kitabu cha Matukio Makubwa yanayotokea Duniani, ‘Guinness Book Records’. Tamasha hilo liliandaliwa na kampuni ya simu za mkononi Vodacom Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...