Wafanyakazi wa Blue Pearl Hotel & Apartment wakijiweka sawa kwa maonyesho ya HARUSI ndani ya Diamond.
Mmoja wa waliotembelea maonyesho ya HARUSI kwenye ukumbi wa DIAMOND JUBILEE wakisiliza maelezo toka kwa washiriki wa maonyesho hayo.
Maonyesho ya Harusi yaliosubiriwa kwa hamu na wadau mbalimbali wa masuala ya harusi na watarajiwa wa harusi yameanza leo katika ukumbi wa DIAMOND JUBILEE huku yakiwa na washiriki zaidi ya 51 waliochukua mabanda kwa kuonyesha na kuuza biashara zao.
Wakizungumza kkwa nyakati tofauti tofauti washiriki hao ambao wamejitokeza kwa wingi, waliyasifu maonyesho ya mwaka huu na kusema kuwa yamekuwa hai na mvuto wa aina yake, kwa kuwa mambo mengi yameongezeka kwa mwaka huu.
"tulishiriki mwaka jana, na mwaka huu pia, ila mwaka huu yamekuwa mazuri zaidi na yenye kupangiliwa zaidi, kwa kweli waandaaji wamejipanga vilivyo" alisema mmoja wa washiriki toka kampuni ya picha ya GRM.
Maonyesho ya mwaka huu yameongezewa ladha kwa kuongezewa vitu mbaliombali, ambapo mbali na kuongezeka kwa nafasi na mabanda, pia kuna upya wa vitu kama 'mdahalo wa Harusi' ambapo wataalamu waliobobea katika masuala ya harusi watazungumza na wale watakaotembelea maonyesho hayo.
Huku jarida la kwanza na la aina yake la kitanzania 'HARUSI MAGAZINE' chini ya usimamizi wa mbunifu wa mavazi maarufu nchini Mustafa Hassanali likisambazwa ukumbini hapo kwa toleo lake la kwanza.
Wadau wote na wakaazi wa jiji la Dar ess salaam wanakaribishwa sana katika maonyesho haya ya siku tatu yanayoendelea ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee.
No comments:
Post a Comment