Marquee
tangazo
Friday, April 1, 2011
MREMBO JULIETH AKABIDHI FEDHA KWA WANAFUNZI WALEMAVU WA NGOZI
MISS Progress Internatinal Julieth Wiliam Lugembe ambaye ni mkurugenzi wa Progressive Foundation, ametoa shilingi milioni 1.4 kwa walemavu wa ngozi wa Wilaya wa Ilala.
Julieth alikabidhi fedha hizo kwa mmoja wa wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi mbele ya mwakilishi wa afisa wa ustawi wa jamii manispaa ya Ilala Rachel Katemi.
Fedha hizo alizitoa kwa ajili ya kununua sare za shule za watoto hao wa shule za msingi wapatao 30.
Mrembo huyo ambaye ni mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Progress Foundation amejitolea fedha hizo kutoka mfukoni mwake ili kusaidia watoto hao.
Julieth alisema kuwa ameamua kuwasaidia watoto ili wapoate elimu bora kama ilivyo kwa watoto wengine wasio na ulemavu.
“Lengo langu ni kuwasaidia watoto wenye ulemavu ili waweze kufikia malengo yao ya kielimu kama wototo wengine ambao hawana ulemavu wowote,” alisema Julieth.
Mlimbwende huyo alitwaa taji hilo la Miss Progress Internatinal katika shindano lililofanyika nchini Italia baada ya kuwashinda warembo wengine kutoka nchi zipatazo 60.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment