Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, May 5, 2012

MAMA SALMA NA WAKE WA MAKAMU WA RAIS WATEMBELEA KAMBI YA TIMU YA NETIBOLI YA TAIFA "TAIFA QUEENS"






Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, Salma Kikwete, akiwapa somo la kucheza na kufunga magoli wakati alipowatembelea kwenye kambi yao ya mazoezi wakijiandaa kwa michuano ya Afrika itakayofanyika hapa nchini hivi karibuni.

Mwenyekiti wa WAMA, Salma Kikwete, akimkabidhi mchango wa shilingi milioni kumi, Mwenyekiti wa CHANETA, Anna Bayi, kwa ajili ya maandalizi ya timu ya taifa ya mchezo huo. Makabidhiano hayo yalifanyika huko Kibaha tarehe 4.5.2012 ambako timu hiyo imeweka kambi.

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Salma Kikwete, akifuatana na wake wa Makamu wa Rais,Zakhia (wa pili) na Asha Bilali (wa mwisho) wakiagana na wachezaji wa timu ya Taifa ya Netiboli huko Kibaha tarehe 4.5.2011. PICHA NA JOHN LUKUWI

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...