Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, May 12, 2012

MVUA YAVURUGA MECHI YA TAIFA QUEENS NA BOTSWANA TAIFA

Maofisa wa kampuni ya Superdoll, Jamal Bayser kulia na Ibrahim Juma kushoto wakisubiri mechi hiyo.

MECHI ya mwisho ya mashindano ya Afrika ya Netiboli yanayofikia tamati leo Dar es Salaam, kati ya wenyeji Tanzania na Botswana imechelewa kuanza kutokana na mvua inayoendelea kwenye Uwanja wa Taifa.
Mgeni rasmi, mke wa makamu wa rais, mama Bilal na mke wa Waziri Mkuu mama Pinda hawajafika bado. Tayari CHANETA imeamua mechi zihamie Uwanja wa ndani wa Taifa.
Mechi hiyo ilipangwa kuanza saa 7:00 mchana na Tanzania ikishinda itakuwa mshindi wa pili, wakati Malawi tayari wametetea ubingwa wao kwa kushinda mechi zote.
Gwiji wa mpira wa kikapu Tanzania Saleh Zonga kulia

Wachezaji na maofisa wa Zambia

Wachezaji wa mabingwa wa Afrika Netoboli, Malawi 

Mtoto wa beki wa Azam FC, Joseph Owino aitwaye, Perrie, aliyezaa na mcheza netiboli Sofia Komba, naye anaisubiri kwa hamu mechi

Taifa Queens wamepasha hadi wamechoka

Katibu wa CHANETA, Rose Mkisi kaamua kutulia tu

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...